Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Julai 12, 2021

Jumatatu, Julai 12, 2021,
Juma la 15 la Mwaka

Kut 1: 8-14, 22;
Zab 124: 1-8 (K) 8;
Mt 10: 34 - 11: 1.


MFUASI WA KRISTO!

Karibuni sana wapendwa kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Tafakari yetu ya neno la Bwana katika somo la kwanza, tunakutana na habari za ujio wa kiongozi asiyemtambua Yusufu, hivyo wana wa Israeli wanaanza kupewa mateso. Kiongozi huyu hakuhangaika kuulizia juu ya wema wote Yusufu alikuwa amewatendea Wamisri enzi za uhai wake. Hivyo aliwaona kama tishio kwa ustawi wa Wamisri, hakujua kwamba wana wa Israeli wangeweza tena kuwa msaada kwa taifa la Misri kama alivyokuwa Yakobo.
Yeye aliwaona kuwa tatizo na hivyo anataka waondoke. Lakini ukweli ni kwamba kadiri alivyoendelea kuwanyanyasa ndivyo walivyozidi kuongezeka idadi yao. Mungu ndiye aliukumbuka wema wa Yusufu kwa taifa la Misri na ndio maana alizidi kuwabariki watu wake waliokuwa wakinyanyaswa na Farao.
Chuki iliyomkumba Farao ndiyo inayotukumba na baadhi yetu pia. Wapo baadhi yetu tusiohangaika kuangalia historia, baadhi yetu tukichaguliwa viongozi tunajidai kuja na mambo mapya, tunaondoa kila kitu cha zamani bila kuangalia sadaka iliyofanywa na waliotutangulia kuhusu kuufikisha uongozi wetu pale ulipofikia. Hii ni sababu za baadhi yetu kulaaniwa. Tusikubali kudharau sadaka au michango iliyofanywa na wale waliotutangulia. Tukidharau mchango wao, Mungu ndiye atakayewakumbuka na kuwasaidia kama alivyozidi kuwasaidia wana wa Israeli. Tuwe watu wa kutambua historia za waliotutangulia.
Katika somo la injili, Yesu anasema kwamba hakuja kuleta amani duniani bali upanga. Na yule ampendaye mwana au binti kuliko yeye hakika hamstahili. Injili ya Bwana, pale tunapoanza kuishi, lazima itawasha moto tu. Kwanza itawasha moto ndani ya mioyo yetu ikitutaka tubadilike, halafu itawasha moto ndani ya uhusiano wa wale tunaokaa nao, lazima itatutaka turekebishe mahusiano yetu na wenzetu ili tusiwe watu wa kulelea uovu.
Huu ndio moto ambao kila mmoja lazima aukubali uwake ndani yake na pia kati ya mahusiano yake na wenzake na ndipo kweli tutaweza kumpenda Yesu. Bila kufanya hay

Sala:
Ee Yesu nisaidie niweze kukufuata kwa moyo wote.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni