Jumapili. 05 Mei. 2024

Tafakari

Jumatano, Disemba 21, 2016

Jumatano, Desemba 21, 2016,
Juma la 4 la Majilio

Wimb 2: 8-14;
Zab 33:2-3, 11-12, 20-21;
Lk 1: 39-45.


MAISHA YETU WIMBO WA FURAHA

Leo katika somo la kwanza kutoka katika kitabu cha wimbo Uliobora, ni Wimbo wa shairi unaovutia kusikia na kuona. Wapendwa wote wawili wanaimba kwa furaha juu ya furaha yao watakayo kuwa nayo watakapo kuwa pamoja. Lakini lazima kusubiri. Muda bado. Injli ya leo ni kioo cha wimbo wa upendo. Ni ujumbe wa upendo ambao unakuwa kati ya mama na mtoto aliyembeba. Elizabeth alisubiri kwa miaka mingi kupata mtoto. Maria, msichana mdogo ana miezi tu sio miaka ya kusubiri ili ahadi yake itimizwe. Salamu ya Maria, kuruka kwa kichanga na wimbo wa Elizabeti unatangaza ukweli wa ahadi ya Mungu.

Ni rahisi kuona ukweli wa furaha ya Elizabeti kutoka moyoni anavyo kutana na Mama wa Mungu na Bwana akiwa ndani ya tumbo la Mama yake Maria. “Hii inakuwaje initokee mimi, hata Mama wa Bwana wangu anitokee mimi”? Mstari huu unaonesha furaha ya kweli ya Elizabeth kukutana na Maria na anaona tendo hili kuwa ni Baraka kubwa ya kukutana na Mama wa Mungu. Ni dhahiri pia kwamba sio Elizabeth tu alifurahi bali hata Yohane Mbatizaji aliyekuwa katika tumbo la Mama yake, anajazwa na furaha pia na anaruka kwa furaha. Ni furaha ghani isio na kifani inayowatokea Elizabeth na mtoto wake ambaye hajazaliwa bado. Je, tunafurahia uwepo wa Kristo anapokuja kwetu? Kama Elizabethi na Mwanaye waliweza kuhisi uwepo wa Bwana, je, sisi hatuwezi kuhisi uwepo wake? Tunapo ingia kanisani, je tunahisi uwepo wa Mungu mara moja? Je, tunahisi utakatifu wake? Na tunapo mpokea Bwana katika komunyo takatifu tunahisi uwepo wake? Je, mioyo yetu ipo tayari kumpokea tena Masiha anayekuja kwetu? Hii inatakiwa kuwa na Imani na inachukuwa jicho ambalo limeelekezwa kwa ujio wa uwepo wa Bwana. Noeli inapokaribia, sisi pamoja na wapendwa hawa, Maria na Elzabeti tuimbe wimbo wa matarajio ya furaha.

Sala: Bwana, natamani kukuona wewe na kuku fahamu wewe. Ninaomba nitambue uwepo wako kati yangu. Nisaidie mimi, niweze kuwa makini hasa, katika uwepo wako katika komunyo takatifu. Ninaomba moyo wangu uruke kwa furaha daima unapokuja kwangu katika hali hii kamilifu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni