Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Aprili 02, 2021

Ijumaa, Aprili 2, 2021
Juma Kuu

IJUMAA KUU

Isa 52:13-53;
Zab 31:2,6,12-13,15-17,25
Ebr 4:14-16, 5:7-9;
Yn 18:1 - 19:42


MTAZAMENI MTU!

Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu. Leo neno la Bwana bado linazidi kututafakarisha juu ya habari za Kristo mfufuka na leo katika Injili Yesu anawatokea wanafunzi wake wakiwa katika kuvua samaki. Wanakwenda kuvua usiku kucha hawapati kitu lakini Yesu anakuja kwao na kuwaelekeza jinsi ya kufanya na wanavyomtii wanafanikiwa.
Jambo la namna hii si mara ya kwanza kutokea kwa hawa wanafunzi. Tukumbuke kwamba Simoni Petro alipokutana na Yesu tena kwa mara ya kwanza ilikuwa tena katika tukio la kuvua samaki ambapo walikuwa wamejitahidi kuvua bila mafanikio lakini Yesu alipomuelekeza basi aliweza kuvua samaki wengi ajabu (Luka 5:1-11).
Sasa anawatokea wanafunzi wake kwa mtindo tena wa namna hii. Hapa alitaka kuwaambia wanafunzi wake kwamba hata baada ya kuondoka kwake miongoni mwao, bado itawabidi wamwite aje kuwasaidia. Watapaswa kulitumainia jina lake na kumwita. Tukumbuke kwamba walipoanza kuvua samaki, walianza tu hivi hivi, hawakuwa wameona hata haja ya kukumbuka kumwomba yule Yesu ambaye hapo kwanza aliwawezesha kuvua samaki wengi ajabu. Sasa anataka kuwaambia kwamba hata baada ya kuondoka kwao kati yao, itawabidi waliite jina lake ili waweze kufanikiwa. Wasipofanya hivyo kamwe hawatafanikiwa.
Mitume katika somo la kwanza sasa wanaonesha kwamba wameelewa somo hili-kwamba jina la Yesu italibidi kuliita, lije lifanye kazi kati yao hata baada ya Yesu kuondoka kati yao na kwa kweli walipojaribu lilifanya kazi kubwa ya kumponya huyu kiwete na leo Petro anaonekana kuelewa hili kwa kusema kwamba Yesu ndiye aliyewezesha kufanya maajabu yote hayo, yeye ni jiwe walilolikataa waashi lakini ndilo jiwe kuu la msingi. Hivyo, anaonesha hadharani kwamba jina la Yesu ndilo jiwe lenye nguvu na lapaswa kutumainiwa.
Ndugu zangu, hapa tunapata fundisho kubwa sana. Je, sisi tunasadiki hilo? Mara ngapi tumeanza kazi au masomo au shughuli zetu bila kusali? Hivi tunafikiri kwamba tukimshirikisha Yesu kwenye shughuli zetu tutachekwa na wengine? Tunataka tufanye wenyewe ili tujisifu ati tumefanya wenyewe bila kumshirikisha Mungu? Ndugu yangu, duniani kuna shida nyingi, mizingo ni mingi, nakwambia hatutaweza kuibeba wenyewe. Tumwite Yesu atusaidie kubeba. Hata kama unaenda hospitali yabidi kuwaombea hata wale madaktari waongozwe na Roho watambue ugonjwa wako. Usifikiri kwamba ati madaktari ni kama miungu inayojua kila kitu. Hata nao ni binadamu na wanatenda makosa makubwa sana wakati mwingine. Unaweza kwenda hospitali halafu anakutendea kosa kubwa na linakupatia madhara makubwa, anaweza hata kukupatia dawa zisizo sahihi, hivyo lazima umwombee hata anapokutibu. Yeye sio malaika.
Hata madereva wanaotuendesha. Tuwaombee jamani, hata nao ni binadamu, mfano wakati anakuendesha gafla akashikwa na ugonjwa wa moyo au kifafa au akarukwa na akili, wewe uliwahi kufikiri hilo? Au hata unapoenda kula hotelini wewe unafikiri kwamba huwezi kukuta labda hata mpikaji alikuwa hata na sumu ya panya nyumbani na kwa bahati mbaya ikamwagikia hata kwenye mchele bila yeye kutambua? Mambo kama haya hufikiriagi? Yeye ni binadamu na chochote chaweza kutokea. Hivyo, lazima kumwomba Mungu kila wakati kila tuendapo na popote tuingiapo.Tumsiifu Yesu Kristo.

Maoni


Ingia utoe maoni