Jumapili, Machi 14, 2021
Machi 14, 2021.
------------------------------------------------
JUMAPILI, DOMINIKA YA 4 YA KWARESIMA
Somo la 1 : 2 Nya 36:14-16, 19-23 ilikuwa ni kwasababu ya dhambi, Mungu aliruhusu Wana Waisraeli wapelekwe utumwani Babuloni. Lakini huruma yake inaonekana kwa wao kurudi katika nchi yao
Wimbo wa katikati: Zab 137:1-6 “ulimi wangu ugandamane na kaa kaa la kinywa changu, nisipo kukumbuka.”
Somo la 2: Efe 2:4-10 Mt. Paulo anatupa somo kuhusu ukombozi. Sio kwa nguvu zetu wenyewe kwamba tulikombolewa lakini ni kwasababu ya huruma ya Mungu. Na hili sio mastahili yenu bali ni kwasbabu ya ni zawadi ya Mungu kwetu.
Injili: Yn 3:14-21 Yohane anaongea kuhusu upendo ulivyo mkubwa wa Baba kwetu sisi. Huu upendo ni mkubwa sana kiasi ambacho alimtuma Mwanae ulimwenguni, si kuuhukumu ulimwengu, bali amekuja kuukomboa na kuwa mwanga wa maisha yetu.
------------------------------------------------
KWA KUWA MUNGU ALIMTUMA MWANAE
Nikweli Kwamba kipindi hiki cha kwaresima tunapaswa kuwa na hakika kuhusu hali yetu ya dhambi na kumrudia Mungu, kwa kufanya mapinduzi ya kweli ya kiroho. Lakini tutakuwa tunakosea kama hatutaweka hali hii katika kiini cha Mungu kuja kwa upendo wake na kutaka kutukomboa sisi wote "jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanae wa pekee ili aje ulimwenguni si kuuhukumu bali kuukomboa ulimwengu, na kila atakaye mwamini hatapotea bali atakuwa na uzima wa milele”.
Injili ya leo inatoa muhtasari wa Injili yote. Inatupa ukweli katika hali nne, kwanza kabisa Baba wa mbinguni anatupenda sisi. Tunalitambua hili lakini hatuweze kuelewa kabisa kwa undani ukweli huu. Mungu Baba yetu anatupenda sisi kwa upendo usio na kikomo na mapendo yalio kamili. Ni upendo ndio uliobeba maana halisi zaidi ya kile ambacho twaweza kufikiri katika maisha yetu. Upendo wake ni kamili.
Pili, upendo wa Mungu ulidhihirishwa kwa njia ya Mwanae wa pekee. Mwana ana maanisha kila kitu kwa Baba, na upendo wa Mwana kwetu unadhihirisha kwamba Baba ametupa yote. Alitupa maisha yake kabisa kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo.
Tatu, jibu zuri ambalo sisi tunaweza kulidhihirisha ni kwa njia ya Imani yetu. Tunapaswa kukubali nguvu ya kubadilisha ya Mwana katika maisha yetu. Tunapaswa kuona zawadi hii kama zawadi kubwa kuliko yote ile ambayo tunaweza kupata. Tunapaswa kumwamini Mwana kwa kumpa maisha yetu kama zawadi.
Nne, matokeo ya kumpokea yeye na kumpa maisha yetu kama zawadi ni kwamba tunakombolewa. Hatuta angamia kwa dhambi zetu, bali tutapokea uzima wa milele. Hakuna njia nyingine ya wokovu isipokuwa kwa njia ya Mwana. Tunapaswa kutambua hili na kukumbatia ukweli huu.
Mt. Teresa wa Mtoto Yesu, alikuwa daima akitazama makosa yake na kuogopa daima kumkosea Mungu. Na katika maandishi yake amesema. “Yesu hana haja na kazi zetu, anachohitaji ni upendo wet tu”. Ukweli huu uliangaza moyo wake uliojeruhiwa, na kumjaza Amani. Akiwa mtoto mdogo aliyafanya haya na kumpatia Mungu maisha yake na kutegemea huruma yake. Mt. Paulo analiweka hili vizuri sana kwa kusema “ni kwa neema ya Mungu tumekombolewa kwa Imani, sio kwa kitu chochote kwa nguvu zetu bali kwa zawadi ya Mungu”.
Tukiwa tunaingia katika hatua hii katika kipindi chetu cha safari ya Imani kwa kipindi hiki cha Kwaresima tunapaswa kujiuliza: Hivi Mungu atakuwaje hivyo mwema kwangu mpaka akamtoa Mwanae wa pekee? Hakuna hukumu katika hili ni furaha yake yakutaka kutukomboa sisi. Ni kwa jinsi ghani jambo hili lilivyo zuri kama (mimi na wewe) tuta amini upendo huu! Kama Mt. Teresa, ua la Kristo, tutatamani kujiweka katika mikono ya Mungu anayetupenda, kama Yesu mwenyewe ni lazima nami niruhusu kuinuliwa na kuruhusu maisha yangu yalete wokovu kwa wengine.
Sala:
Bwana, ninajitoa kwako kama mtoto mdogo katika mapendo yako.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni