Jumatatu, Januari 25, 2021
Jumatatu , Januari 25, 2021,
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
Sikukuu ya kuongoka kwa Mt. Paulo, Mtume
Mdo 22: 3-16;
Zab 117: 1-2 (R.) Mk 16:15
Mk 16: 15-18.
KUKUTANA NA YESU!
Habari ya Paulo ni kuhusu yeye kukutana na Yesu. Baada ya kukutana na Yesu, hakuhitaji kitu kingine zaidi. Hakuna kazi iliokuwa ngumu sana wala jaribuu kubwa sana la kumshinda. Injili ya leo imetoka katika sehemu ya mwisho ya Injili ya Marko. Na inaeleza kuhusu maelekezo anayo wapa Yesu wafuasi wake kabla hajaondoka kwa mara ya mwisho. Ni maneno yanayo ingia sana kwa Paulo. Yanaanza na maelekezo ya kutangaza habari njema kwa kila kiumbe. Hili ndilo alilokuwa akilifanya Paulo baada ya kufika kwa watu wa mataifa, kupita kote huko ambako kwa sasa kunaitwa, Uturuki, kupitia Ugiriki na makedonia na mpaka Roma. “Watakao amini na kubatizwa wataokolewa”. Paulo aliishi vyema mpaka akifikia kusema “sio mimi naishi bali ni Kristo anaishi ndani mwangu”. Alama ya muunganiko kamili na Bwana.
Kuongoka sio kitu kinacho tokea mara moja katika maisha. Ni kitu ambacho kinatokea kwetu mara nyingi katika maisha yetu. Tuwe tayari kujibu kila wakati Bwana wetu anapotuita kwa kitu kikubwa zaidi. Tunaitwa kufungua macho ya mioyo yetu. Tunaitwa kutambua upofu wetu kwenye wito wa Yesu, na kujiandaa kwa toba ya kweli. Kwani Yesu anataka kututuma kila mmoja wetu Ulimwenguni kote kuhubiri habari njema ya msamaha na kuendeleza kazi ambayo yeye ameianzisha ulimwenguni.
Sala:
Bwana, ninaomba nikubali kama Paulo, wito wako wa kukutana na wewe. Ninaomba nikaribishe wito wako kwa moyo wazi. Ninaomba niendelee kutembea katika njia za wito wako siku zote za maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni