Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Januari 01, 2021

Ijumaa , Januari 1, 2021,

SHEREHE YA MARIA, MAMA WA MUNGU

Hes 6:22-27;
Zab 67: 1-2, 4, 6-7;
Gal 4:4-7;
Lk 2:16-21

MAMA MARIA, MLINZI NA KIONGOZI WETU!

Katika somo la kwanza, baraka ya Mungu kwa watu wake imeainisha tumaini kwao. Ilimaanisha ushujaa wa kuyashinda matatizo ya kila siku za maisha. Leo sisi pia tunaobwa tutumaini katika Bwana na kuomba baraka zake mwanzo wa mwaka huu. Katika somo la pili, Paulo anatupatia sisi sababu za kuwa na tumaini katika mwanzo wa Mwaka Mpya: Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, ambaye amekuwa mmoja pamoja nasi; alikuwa kaka yetu, katika kila kitu kama sisi isipokuwa katika dhambi. Mungu ametukubali sisi kama watoto Wake. Sisi Wakristo tunapaswa kushuhudia upendo wa Mungu ukidhihirishwa kwa Yesu Kristo. Pia leo, Kanisa linasherehekea sikukuu ya Maria, Mama wa Mungu. Mama Kanisa anajali sana kiasi cha kuwa na mfano ulio bora wa kuigwa kwa mwaka mzima na hivyo anatupa sisi Mariamu, Mama wa Yesu katika siku ya kwanza ya mwaka. Kadiri siku inavyoanza na Mwaka Mpya unaanza, sisi hatupo pekeyetu; tunaye Mama Mkombozi ili atulinde na atuongoze sisi kwa mwaka wote.

Ndani ya Yesu kuna asili mbili – ya kibinadamu na ya kimungu, lakini yeye ni mtu mmoja. Mariamu ambaye pia ni Mama wa Mungu. Alikuwa na nafasi ya pekee sana ya kuutoa mwili na damu yake kwa Yesu. Mariamu anachukua nafasi katika kazi ya ukombozi kazi ya Kristo pamoja na upendeleo wa pekee kiasi cha kuwa hata malaika wa mbinguni wangekuwa na wivu. Kati ya viumbe vyote vya Mungu ulimwenguni na mbinguni, hakuna hata mmoja aliye mtakatifu sana na aliye karibu sana na Yesu zaidi ya Mariamu, Mama Yake. Mama Maria ni Eva Mpya. Eva, mama wa wanadamu alileta kifo kutokana na kutokutii kwake, kwake yeye mwenyewe na kwa wanadamu wote, lakini Mariamu Eva Mpya, alileta uhai kutokana na kutii kwake. Mt. Ireniusi alimuita Mariamu kuwa ndiye chanzo cha Ukombozi wetu. Kadinali Newman aliyetoa tofauti kati ya Mariamu na Eva alisema, “Kama eva alivyoipoteza nafasi ya upendeleo kutokana na Dhambi, hivyo Mariamu aliipata nafasi ya upendeleo kutokana na matunda ya neema; Kama Eva alivyokosa kutii na asiyeamini, hivyo Mariamu alikuwa mtii na aaminiye; kama Eva alivyokuwa ni chanzo cha kuanguka kwa wote, Mariamu alikuwa ni chanzo cha ukombozi kwa wote; kwamba Eva aliandaa mazingira ya kuanguka kwa Adamu, hivyo Mariamu aliandaa mazingira ya kuweka hali sawa kwa Bwana; hivyo, ambapo zawadi ya bure haikuwa ni dhambi bali ni bora zaidi, inafuata kuwa, kama Eva alisaidia katika kutekeleza dhambi kubwa, Mariamu alisaidia katika kutekeleza kile kilicho bora zaidi. Mariamu ni zawadi kubwa sana kutoka kwa Yesu kwetu sisi. Yesu alifahamu kuwa Mama Yake alikuwa mkuu na kama ni zawadi ya mwisho, alimtoa Mariamu kwetu sisi kama mama yetu.


Sala:
Mariamu, nifundishe mimi kusema Ndiyo kwa Bwana.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni