Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Disemba 06, 2020

Desemba 6, 2020.
------------------------------------------------
DOMINIKA YA 2 LA MAJILIO

Somo la 1: Is 40:1-5, 9-11 Mungu anamwambia Isaya awafariji watu wake, lakini pia anawaambia waandae njia kwa ajili ya ujio wa Bwana, Mungu anakuja kuwaokoa watu wake

Wimbo wa katikati: Zab 84:9-14 Bwana ni mwenye huruma, sauti yake inaongea Amani, na msaada wake ni kwa wale wote wanao mtii. Kwake huruma na uaminifu nimekutana, haki na Amani vimekumbatiana.

Somo la 2: 2Pet 3:8-14 kama Paulo, Petro anaamini kwamba Yesu atakuja muda sio mrefu, wakati usiotarajiwa, hivyo wote wanapaswa kujiandaa. Kama Bwana anakawia kuja, ni kwasababu anawapa watu muda wakutubu na kuwa tayari kukutana naye atakapokuja.

Injili: Mk 1:1-8 Marko anafungua injili yake kwa taswira ya Yohane akitangaza umuhimu wa watu kutubu na kubatizwa kwa ajili ya ujio wa Masiha anayekuja katika maisha yao.

------------------------------------------------

MAJILIO: ANDAA NJIA YA BWANA

Mtu mmoja alikuwa na saa kubwa ya gharama sana iliyotengenezwa Switzerland. Aliiweka dirishani, sehemu ambayo ilionekana na wote waliokuwa wakipita njia na wengi walirekebisha majira ya saa zao kwa kutazama saa hii. Lakini siku moja saa ilipata shida Fulani. Ilianza kuonyesha saa ambayo sio. Hivyo mwenye saa kila siku alitumia nguvu nyingi na muda mwingi kuwa karibu na saa ili aiweke kwenye wakati unaotakiwa. Hali hii iliendelea kwa miaka. Siku moja mtu alimfuata akamwambia kwanini “badala ya kutumia nguvu nyingi na muda wako mwingi kuweka saa hii kwenye wakati sahihi kila siku, kwanini usirekebishe vifaa vya ndani?” Yule mwenye saa alifurahi kwani hakuwahi kufikiri hivyo. Sisi nasi tuonaogopa kubadilika kutoka ndani kwani tunaogopa kuonakana vibaya machoni pa watu au pengine tutapoteza umaarufu wetu kwasababu watu wameshatuona kama watu wenye saa ya gharama hivyo tunafanya kila jitihada umaarufu wetu usipotee, na hivyo tunateseka kweli. Kwanini tusibadilike kutoka ndani na kuanza kufurahia maisha kama yalivyo?

Mungu hakumtuma Mwanae aje abadili watu wachache. Alimtuma Mwanae awabadili watu wote na ubinadamu wote. Ndio maana kila majilio tunakutana na Yohane Mbatizaji akitutangazia ujio wa ukombozi wa wanadamu wote. Anawaambia watu “kuanda njia kwa ajili ya ujio wa Bwana”. Lakini kwanini tunahitaji kujiandaa kwa jili ya Bwana?

Siku moja mtu mmoja alivyutwa na jagi nzuri aliloona sokoni. Alilinunua na kwenda nalo nyumbani. Baada ya kuliweka sebuleni na kutazama nyumba yake alitambua kwamba lile jagi lake lilikuwa nzuri sana kuliko nyumba yake na hivyo akaamua kupaka rangi nyumba yake. Na kununua kateni nzuri za rangi zuri, na kununua makochi na kupendezesha nyumba yake. Kwa njia ya jagi lile nyumba nzima ilibadilika na kuwa nyumba mpya. Wakati Yesu anapo ingia katika maisha yetu anabadili kila ktiu. Kila kitu ambacho kinahitaji kubadilika kitaonekana dhahiri. Tunapo sogea karibu zaidi na Mungu ndivyo tunavyozidi kujiona tulivyo na kuona utofauti wetu! Na hii ndio maana tunayohitaji kuandaa njia kwa jili ya Bwana.

Majilio ni kipindi cha kungojea ujio wa Bwana, na Bwana pia anatusubiri kurudi kwetu kutoka kwenye dhambi. Mungu wetu anatupenda sisi na upendo wake unatufanya sisi tumtafute yeye. Mungu alienda kuwatafuta adamu na Eva katika bustani ya edeni, wakati wakiwa wamejificha, walijificha baada ya kujua kwamba wameenda kinyume na kazi ya Mungu. Wakati mwingine sisi tunalalamika Mungu amejificha mbali na uso wetu, na kwamba haonekana lakini katika hali ya kweli sisi ndio tuliojificha kutoka kwake? Na hivyo Mungu akauliza swali: “upo wapi” ni Mungu mwenyewe aliye anza kutafuta, kwa upendo wake kwetu. Agano lote la kale ameendelea kumtafuta Mwanadamu na kumleta kwenye upendo wake. Je, tupo tayari kumkaribsha yeye katika maisha yetu?

Katika somo la kwanza tunasikia kwamba “andaa njia katika jangwa, Bwana anakuja. Fanya njia iliyo nyooka Bwana wetu anakuja”. Ni katika mioyo yetu tunapaswa kufanya njia iliyo nyooka kwa ajili ya Mungu. Ni mabonde ya dhambi katika mioyo yetu yanapaswa kusawazishwa kwa huruma na uponyaji wa Mungu, na vilima vya majivuno ndani ya mioyo yetu ambavyo vinapaswa kusawazishwa. Somo la pili linatukumbusha kwamba tunaishi katika kipindi cha huruma, wakati tukiwa na muda wa kutubu. Yohane Mbatizaji kama Isaya anasema “ tengeneza njia ya Bwana” “tengeneza njia iliyo nyooka” maisha ya dhambi na vishawishi yaachwe. Sawazisha vilima vya ubinafsi na kujaza mabonde ya utupu kwa sala na fadhila. Njia zisizo nyooka zinapaswa kunyooshwa kwa ukarimu na kujali.

Maandalizi yetu ni muhimu tuangalie mioyo yetu na kumkaribisha Mungu katika maisha yetu, na uponyaji wake ili Roho Mrtakatifu atufanye viumbe vipya. Toba inaanza kwa kutambua umuhimu wa kumpokea Mungu, kwa kujitazama sisi ni nani na tupo kwa ajili ya nini, pia kutazama jitihada zetu za kumfuata Kristo. Ni kutambua uhaba wetu wa kiroho na kumfuata Yesu mkombozi wetu, na ambaye anatupatia nguvu ya kukuwa katika mapendo. Noeli itakosa maana kama hatutaandaa njia katika mioyo yetu kwa ajili ya Bwana. Wakati huu wa majilio, tujiulize hivi ni dhambi gani inaniweka mbali na Mungu? Tuuungame na kufanya toba ili upendo wa Mungu utukute sisi.

Sala:
Ninakushukuru Bwana, kama Mchungaji mwema unatulisha sisi, unatukusanya kama Mchungaji ukituchukua kifuani pako kwa uangalifu. Njoo Bwana Yesu! Ninatamani kubaki katika mikono yako kwa milele yote. Bwana, tunaomba tuone ukarimu wako, tujalie ukombozi wako. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni