Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Disemba 03, 2020

Desemba 3, 2020.
ALHAMISI, JUMA LA 1 LA MAJILIO


Somo la 1: Is 26:1-6 Isaya anawasihi watu wake waweze kumtumainia Bwana daima, kwani yeye ni Mwamba wa milele. Anawashusha wakuu na kuwapasndisha masikini. Israeoi wanamuimbaia Bwana afungue milango, kwa taifa lenye haki liingie.

Wimbo wa katikati. Zab: 117:1,8-9,19-21,25-27 Mzaburi anamuuliza Bwana afungue milango, ili taifa lenye haki liingie. Inasifu na kusema ni vyema kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wakuu..

Injili: Mt 7:21, 24-27 Yesu anawaambia wafuasi wake, ni kwa wale tu wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni wataingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa Bwana pekee palipo na msingi wa Imani yetu.

------------------------------------------------

Ndugu zangu wapendwa karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Isaya katika somo la kwanza anatabiri kwamba taifa lishikalo haki na kweli ndilo litakalofunguliwa mlango. Anaendelea kusema kwamba amtumainiaye Bwana hakika atalindwa lakini wenye majivuno, waliojipandisha juu; hakika atawashusha.

Katika injili ya leo, tunagundua kwamba Yesu alipokuja duniani kwa mara ya kwanza, aliuunga mkono ujumbe huu wa Isaya kwa kusema kwamba yule ayafanyaye mapenzi ya Mungu ataingia katika ufalme wa mbinguni na anamfananisha na mtu aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba ikaweza kustahimili dhoruba kali. Anawaambia kutimiza mapenzi yake ni kama kujenga juu ya mwamba na hii itakufanya kushinda dhoruba zote na mwishowe nyumba yako itabakia imara. Hivyo, tunapongojea ujio wa pili wa Bwana wetu, tujenge nyumba zetu juu ya Mwamba, yaani Kristo kwa kuwa watu wa haki na kweli. Hivi tutakuwa taifa lake na atatufungulia mlango tupate kuingia aliko.

Maoni


Ingia utoe maoni