Jumapili, Novemba 15, 2020
Jumapili, Novemba 15, 2020.
Dominika ya 33 ya Mwaka A wa Kanisa
SIKU YA MASKINI ULIMWENGUNI
Mit 31:10-13, 19-20, 30-31;
Zab 127:1-5;
1Thes 5:1-6;
Mt 25:14-30
KUTUMIA THAMNI YA VIPAJI VYETU!
Ni bahati mbaya kuona kipaji hakitumiki na kuishia tu hivi hivi, kwani kipaji kinavyo potea na mtu naye hukosa maana. Mchezaji mpira mzuri anaishilia kwenye ulevi, au mwimbaji mzuri anaishilia kwenye madawa ya kulevyia, mwanasiasa mzuri anapotea hivi hivi, na kupoteza kipaji moja kwa moja. Mwandishi mmoja wa Amerika anayeitwa Thoreau anaongelea kuhusu “majukumu ya vipaji”..
Wakati mmoja kulikuwa na mfalme aliyekuwa na watoto watatu, na kila mtoto alikuwa na kipaji cha pekee. Wa kwanza alikuwa na kipaji cha kuotesha miti ya matunda na kuvuna. Wa pili alikuwa na kipaji cha kutunza na kukuza kondoo. Na wa tatu alikuwa na kipaji cha kucheza ala mbali mbali za mziki. Siku moja mfalme alitaka kusafiri kwenda nchi za njee kibiashara. Kabla ya kuondoka akawaita watoto wake watatu pamoja, akawaambia kwamba alikuwa anawategemea kuwafanya watu wakae kwa kuridhika wakati yeye akiwa amesafiri.
Kwa muda fulani mambo yakaenda vizuri. Kukaja kipindi cha baridi, kilikuwa kipindi kibaya kweli. Kulikuwa na ukame wa kuni. Hivyo yule mtoto wa kwanza alikumbwa na changamoto kubwa sana je, aruhusu watu wakate miti mizuri ili wawashie moto? Baada ya kuona watu wanatetemeka baridi akaamua kuwaruhusu wakate miti. Yule wa pili pia alikumbwa na changamoto pia. Kulikuwa na uhaba wa chakula. Je, aruhusu watu wachiche baadhi ya kondoo wake kwa jili ya chakula chao? Baada ya kuwaona watoto wanalia kwa njaa, moyo wake ukavutwa na huruma akawaruhusu watu wachinje baadhi ya kuondooo wajipatie chakula. Hivyo watu wakawa wana kuni na pia chakula cha kupika. Lakini kipindi cha baridi kiliendelea na watu walihisi baridi sana. Walianza kuboreka na hakuna aliyekuwepo kuwaburudisha. Baadae wakamgeukia yule mtoto wa tatu anayejua kucheza ala za mziki ili awaburudishe kwa muziki wafurahi lakini alikataa. Mwishowe watu waliamua kuhama baada ya kuona hali ni mbaya na kwenda kijiji kingine.
Baada ya siku chache mfalme alirudi. Alihuzunika sanaa baada ya kuona watu wake wengi wamehama. Akawaita watoto wake watatu akawaambia kila mmoja asimulie ni kitu ghani kimesababisha haya? Wa kwanza akasema baba nafahamu hutachukia wakati baridi ilivyo ongezeka ilibidi niwaruhusu watu wakate baadhi ya miti ya matunda kwa ajili ya kuni. Alafu wa pili akasema nadhani hutachukia kwani wakati walivyokosa chakula niliwaruhusu wachiche baadhi ya kondoo wajipatie chakula. Badala ya kuchukia baba, baada ya kusikia hivi aliwakumbatia watoto wake wawili kwa furaha.
Watatu akaja mbele ya baba yake akiwa amebeba kinanda. Akasema baba nilikataa kuwachezea muziki kwasababu nilijua haupo ili ufurahie muziki. Akamwambia sawa cheza sasa mziki mzuri kwani moyo wangu una huzuni sana. Yule kijana akaanza kucheza na tazama alishindwa kucheza kinannda kwani alikuwa ameshasahau kwani hakufanya mazoezi hivyo hakuweza. Baba akamwambia kushindwa kucheza ni adhabu yako wala sikuadhibu.
Je, mtoto huyu wa tatu hatukumbushi kuhusu huyu mtoto wa tatu katika mfano wa Yesu kwenye injili? Aliyeficha talanta! Ni wangapi kati yetu tunaweza kusema tumetumia vipaji vyetu vyote kwa nguvu na kwa moyo wetu wote kama wanadamu kwa ajili ya Mungu? Watu wengi wanachezea maisha, kuishi bila malengo, na kufa bila hata ya kutambua utajiri wa vipaji walivyo navyo. Wengine wanafanya kazi nyingi sana lakini kiukweli sio kipaji chao. Wanaweza kuwa wanatafuta mali ya hali ya juu kabisa lakini mwishowe huishia vibaya na kuwaacha wamechoka kabisa. Tunapaswa kuwa makini tusije tukaharibu maana ya mfano huu wa Yesu. Ni katika kuishi tunatambua vipaji vyetu na nikatika kuvitumia vinakuwa. Muda sio mwingi muda wa mavuno utafika kwa kila mmoja wetu. Swali la kujiuliza, je nimetumiaje vipaji vyangu? Kwa ajili yangu au kwa ajili ya wengine pia?
Somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Methali, kinaongelea kuhusu mke mwema anayezaa matunda mema kwa kila kitu. Hakukaa bila kazi, anatumia kila kitu ambacho anapata kwa ajili ya kuongeza mafanikio ya familia. Huyu mwanamke ni wa kuaminika. Wakati akihangaika kwa ajili ya mahitaji ya familia anashugulika pia kwa ajili ya mahitaji yake ya kiroho na pia kwa ajili ya mahitaji ya wengine. Anajitoa kwa ukarimu kwa wale wahitaji, anaongea maneno ya upole, ni hekima tupu inayotoka katika midomo yake. Huyu mwanamke wa pekee ni ishara jinsi tunavyopaswa kuwa kila wakati tukileta mafanikio kwa namna mbalimbali.
Katika somo la pili barua ya Paulo kwa Wathesalonike, Paulo anaendelea kuongelea kuhusu ujio wa pili wa Bwana wetu. Anawaambia kuhusu alichosema Yesu-kwamba ujio wake wa pili utakuwa kama kuja kwa mwizi hakuna ajuae siku wala saa. Lakini hili halipaswa kuwaogopesha kwani wamejiandaa na wanaishi ndani ya Imani ya Kristo.
Mfano wa Injili unatupatia sisi mafundisho manne. Kwanza kabisa, inatuambia kwamba kila mtu Mungu amempatia vipaji tofauti tofauti. Tunaitwa tutumie kikamilifu vipaji tulivyopewa kwa manufaa ya jumuiya yoto ya kibinadamu. Pili, kazi yetu daima haitaisha. Wale watumishi wawili walionyesha tu yale walio pata hakuambiwa kwamba wafanye kazi wakifika sehemu Fulani wapumzike. Lakini kwasababu ya uaminifu wao wanapewa hata majukumu makubwa zaidi. Tatu, mtu yeyote ambaye hatafanya kitu ataadhibiwa. Yule aliyekuwa na talanta moja hakuipoteza. Hakufanya chochote nayo. Kama alikuwa amejaribu na kushindwa angekutana na huruma na msamaha. Hata mtu aliye na talanta moja ya chini kabisa bado ana cha kuongezea. Hapa kuna angalisho sio wale tu wanaotumia talanta vibaya vitaondolewa bali pia wale walio nazo na hawazitumii kuonyesha kazi nzuri. Na mwisho yeyote aliye na zaidi ataongezewa na yule asiye na kitu hata kile anachodhani kwamba anacho kitachukuliwa na kupewa aliye na zaidi. Inaonekana kama vile sio sawa, ni sawa na kumuibia maskini na kumpa tajiri. Lakini Yesu alitaka kutuambia kwamba wale walio wakarimu daima kwa ndugu zao watajikuta daima wanabarikiwa kuliko wale wanaoficha. Wale wanaoficha na kuwa na hofu ya kupungukiwa kuna hatari ya vyote kuchukuliwa na kuondoka bila kujiwekea hazina.
Sala:
Bwana, ninakupa yote ulionipa mimi na ninakushuru kwa yote ulionipa mimi. Ninaomba nitumie yote ulionipa kwa ajili ya utukufu wako na sifa yako ili niweze kujenga ufalme wako. Ninaomba nisijilinganishe na wengine, bali nijikite tu kutimiza mapenzi yako matakatifu.
Amina
Maoni
Chesco Longo
Nimebalikiwa na tafakari ya leoIngia utoe maoni