Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Novemba 08, 2020

Jumapili, Novemba 8, 2020.
Juma la 32 la Mwaka

Hek 6:12-16;
Zab 62:2-8;
1 Thes 4:13-18;
Mt 25: 1-13



TAA ZINAZO WAKA

Somo la kwanza linaimba sifa za hekima. Wakati huo huo linasema kwamba hekima inaweza kupatikana na wale wanayo itafuta. Katika somo la pili Paulo anawafariji watu wa Wathesalonike ambao wana wasiwasi na wapendwa wao ambao walishafariki. Anawaambia kwamba hakika Mungu atawafufufa kama alivyo mfufua Mwanaye Yesu Kristo. Katika somo la Injili Yesu anatuambia tuwe tayari kwani hatujui siku wala saa.


Katika hali ya kwanza kabisa mfano huu unaonekana hautendi haki. Unaonekana sio sawa kwasababu hawa wanawali watano hawakaribishwi katika harusi kwasababu tu, taa zao zimeisha mafuta. Lakini ukweli ni kwamba huu mfano unaenda ndani zaidi ya hilo. Kuna kitu zaidi ya taa za mafuta. tunaweza kuuelezea katika hali ya kisasa kwa namna ifuatayo.


Wale wanawali ni kama wanawake kumi walioenda kwenye duka kununua kitu kwa ajili ya Noeli. Wakaondoka mapema wakiwa na shauku kubwa, sehemu zilizo salama karibu na saloni ya nyewele mjini. Kila mmoja amebeba begi na kulishika vizuri ili asije mtu kumpokonya. Wanawake watano walikuwa na hekima na wakarimu. Walikuwa ni watu wafanyakazi wazuri sana ambao wameshafanya sadaka sana kwa ajili ya kuhifadhi kwa ajili ya kununua. Walitaka kupata punguzo kubwa angalao kwani kila mmoja alikuwa na familia ya kutunza. Walikuwa hawafikirii sanaa juu yao wenyewe bali pia watoto wao na nyumbani kwao. Wengine watano walikuwa ni wajinga na wapumbavu. Hawakuwa na hali ya kuhifadhi kidogo kwa ajili ya nyumbani na watoto. walikuwa wakifikiria tu mambo yao wenyewe.


Stoo ile ya kuhifadhi vitu ilichelewa kufunguliwa. Kusubiri kwao walichoka sanaa. Wanawake wote kumi walilala. Gafla kukasikika sauti. Stoo ilikuwa ikifunguliwa na kila mtu akafanya bidii kuwahi. Hapo ndipo wale wapumbavu walipotambua kuwa wana hela kidogo kwenye pochi zao. Walisahau kwamba wiki iliopita walienda kununua vitu na wakatumia hela nyingi sana kwa ajili yao wenyewe. Katika kuchanganyikiwa wakawarudia wale wenye hekima kuwaomba wawape hela kidogo , tutawapa tukifika nyumbani, wakasema samahani tuna kidogo tu kwa ajili yetu wenyewe. Huu ndio muda wetu tunaweza kukimbia nyumbani mara moja na kirudi, wakiwa wanasema hivi, wale wenye busara wakaenda ndani. Na wale wajinga wakabaki pale njee. Wakachukuwa teksi mara moja kwenda nyumbani. Lakini muda waliofika nakwenda benki wakarudi wakakuta tayari stoo ipo tupu. Mwenye stoo akawaambia samahani sina cha kufanya ni makosa yenu. Kwanini hamkuja kwa wakati? Wakatambua kwamba alikuwa akiwahoji sawa, wakaondoka wakiwa wamechanganyikiwa na bila furaha, kwasababu ya uzembe wao.


Na sasa turudi kwenye mfano wa Yesu. Kwa wale wanawali wenye busara ilikuwa ni muda tuliopewa wakuishi. Ni kitu ambacho walikiishi na kuthamini na kujiandaa. Hali hii haikuwa ni ya kujirudia ili kukutana na Bwana harusi na kuingia karamuni. Hakukuwa na njia yeyote yakuikosa. Kwa wanawali wasio na busara ni tofauti. Wao walichukulia kuwa ni kitu cha kawaida, na kufanya kwa mazoea. Na hivyo wakashindwa kuingia ndani. Lakini ukweli ni kwamba ni mfumo wa maisha yao yote ulikuwa mbaya. Kwa njia nyingine hawakuhukumiwa kwasababu ya kosa moja la maisha yao. Wale wenye busara walikuwa tayari na makini, walikuwa wakiyatenda yote yaliosemwa. Wale watano wengine hawakuwa tayari na wala hawakuwa wamejiandaa, walikuwa wasikilizaji wa maneno tu bila kutenda.


Kwetu sisi somo linaonekana dhahiri. Sisi hatujishughulishi na stoo. kwamba. Ni maisha yetu ya umilele yalio hatarini. Kuna hatari ya kujikuta sisi wenyewe tumefungiwa njee katika karamu ya mwisho. Wakati sauti ya Bwana itakavyo sikika. Yote ambayo atahitaji hatataka kujua ni mtu wa namna ghani, wala sio mimi ni mangapi nilio nayo. Je, itakuwaje tukikamatwa tukiwa hatuja jiandaa? Tunapaswa kukuta daima taa zetu zinawaka. Tunapaswa kuweka mafuta daima. Bwana anaweza kuja wakati wowote.


Lakini tusisahau kwamba tunaalikwa kwenye sherehe ya maana sana. Ni kwenye harusi sio mazishi. Ni furaha sana kwamba wote tuna mwaliko. Kama tumemfanya Yesu ni rafiki katika barabara yetu, ni wazi kwamba siku hiyo haitatukuta bila kujitambua au kujiandaa.


Tunaitwa kushikilia na kubeba mwanga wa Kristo. Lakini ni wazi kama wale wanawali wapumbavu kuna wakati na sisi tunakosa mafuta kwasababu ya kutojishugulisha kwetu mara nyingine. Na kuruhusu taa hii kupungukiwa na mafuta. Kwa njia ya sala na kuwa tayari, Yesu atatusaidia kuhakikisha taa zetu zinabaki zikiwa zinawaka.


Sala:
Bwana tusaidie tuweze kuweka mwanga wa taa ya imani yako ukiwa unawaka daima. Tunaomba tusishikilie kitu kingine zaidi, na kwa kufanya hivyo tuweze kukutana nawe kila unapotuita. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni