Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Oktoba 11, 2020

Jumapili, Oktoba 11, 2020.

Dominika ya 28 ya Mwaka

Isa 25: 6-10;

Zab 22:1-6;

Phl 4: 12-14, 19-20;

Mt 22:1-14

MWALIKO KWENYE KARAMU!

Karamu ya harusi ni picha inayotumika katika Bibilia kuonesha upendo wa Mungu na wana Waisraeli. Katika mfano wa Injili, Bwana harusi ni Yesu, yeye ni Mwana, Bibi harusi ni wanadamu wote ambao Mungu anawapenda sana. Karamu ni furaha ya kuwa na Masiha. Ambaye anakubali Injili na kuingia katika karamu hii huingia na kupata furaha kubwa. Katika Biblia ufalme wa Mungu haufananishwi na kikanisa ambacho watu hkusanyika ili kusali kwa moyo wote. Haulinganishwi na Monesteri Fulani ambayo kuna ukimya na hakuna sauti inayo sikika, na ambapo watu hawasumbui wengine wakiwa wanatafakari na kuzama kabisa, bali ni karamu, ambapo watu wanakutana na kula, kunywa na kushangilia pamoja.

Katika somo la kwanza nabii anatabiri kwamba Mungu ataaandaa karamu ambayo watu watashangilia ushindi kuhusu kifo. Wakati wa Pasaka ni muda wa kushangilia kutokuvunjika kwa uhusiano huu wa Bwana harusi na Bibi Harusi, yaani Kristo na watu wake. Kumbe si hata kifo kinaweza kumtenganisha Bwana harusi huyu na Mpendwa wake. Kuanzia hapo, hakuna tena uchungu, wala kutokuaminiana, wasi wasi kwani kifo cha iana yeyote kimeshindwa, kaburi li wazi.

Watumishi ambao walichukua wito huu wamegawanyika katika sehemu mbili. Wakwanza kabisa ni manabii wa Agano la Kale, hadi Yohane Mbatizaji. Walichukua jukumu la kuwaandaa Waisraeli ili waweze kumpokea Bwana harusi, Yesu. Hawakufanikiwa sana. Kundi la pili ni mitume na sisi wote, matokeo yaliopatikana na wao ni nafuu zaidi.

Walioalikwa wa kwanza hawakuja kwenye karamu, hawakuwa na moyo wa kuacha mambo yao, shamba na biashara. Hawakuhitaji karamu, walijisikia waliojitosheleza, wakiamini kwamba wana kila kitu walicho hitaji katika maisha hivyo hawana shida. Hawa iliwawakilisha viongozi wa dini wa Waisraeli, ambao walikuwa wameridhika na hali ya dini yao ambayo iliwapa nafasi na heshima mbele ya watu, wakijiona mbele ya Mungu ni hivyo hivyo. Wale ambao hawafahamu umaskini wao, ambao hawakusikia kilio kwa ajili ya ulimwengu mpya, hawawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. Watajiweka katika maana yao wanayo ishi. Ni wale maskini tu wanaweza kufahamu hali yao mbele ya Mungu.

Katika Injili, Mwinjili Mathayo, anaweka historia yote ya ukombozi kwa kutumia mfano, mfano unafananisha Ufalme wa Mungu na karamu, kama inavyopatikana leo pia katika somo la kwanza la nabii Isaya, ambalo linatazama Ufalme wa Mungu, kama karamu kubwa ya Bwana ambayo Bwana atawapa watu wake katika mlima mkubwa (Yerusalemu). Ufalme huu wa Mungu unadhihirishwa katika uhalisia-sehemu ambayo kifo kitatokomezwa, na kujazwa na furaha ya watu walio msubiri Masiha aliye ahidiwa tangu kale. Lakini pia Isaya anawakilisha pia ujio wa Masiha kwa karamu-ambapo kila mtu atakuwa na uchaguzi wakuchagua apendacho katika karamu.

Mathayo anaonesha kwamba Ufalme wa Mungu ni kitu ambacho kinapaswa kupokelewa na kukubaliwa. Sio kitu ambacho mtu anakipigania na kukitafuta bali ni kupokea kama zawadi kutoka kwa Mungu, na Mwanae Yesu. Lakini pia maana ya karamu inabadilishwa pia katika hali ya karamu ya mwisho ya Mwana kondoo ambapo hukumu itakuwa kwa Waisraeli. Hawa ni wale watakao hukumiwa kwa kutokupokea ufalme huu wa Mungu kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo. Maada hii inaendelea pia katika jumuiya ya waumini ambao wamepokea ufalme wa Mungu. Hivyo ufalme wa Mungu, ingawaje ni zawadi kwetu, inahitaji mwitikio. Kukubali hili inabidi kuacha maisha ya zamani na kumvaa Kristo kwa maisha mapya au kwa namna nyingine tuvae utu wa Mungu. Kukubaliwa kwetu na Mungu inatagemea sana jinsi tulivyokubali Ufalme wake. Wakati Mungu alivyo niita mimi kumfuata, napaswa kumfuata na kujibu wito wake bila kujibakiza.

Sala:
Bwana, ninakupa wewe maisha yangu. Ninaomba niweze kuwa muwazi kwako kila siku kwa kila njia, nikitafuta kupokea kila neno linalo tumwa kutoka katika moyo wako wa huruma. Ninakuomba nitumiwe nawe niweze kuwa chombo cha huruma kwa watu wote ulimwenguni. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni