Alhamisi, Septemba 24, 2020
Alhamisi, Septemba 24, 2020,
Juma la 25 la Mwaka wa Kanisa
Mhu 1: 2-11
Zab 89: 3-6, 12-14, 17
Lk 9: 7-9
KUTUMIKIA MUNGU NA JIRANI!
Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo basi kanisa linaadhimisha kumbukumbu ya Mt. Vincent wa Paulo anayesifika sana kwa maskini, na masomo yetu yanatuongoza vyema katika kumtafakari Mtakatifu huyu. Somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Muhubiri kinazungumzia kuhusu mhubiri, huyu alishi duniani, akaona jinsi wanadamu wanavyo pambana na kuchoka. Wanavyongangania kupata vitu ambavyo hata baada ya kuvipata hawavitumii au hawavifikishi potpote, anaye hangaika kumdhulumu mwingine lakini kile kitu alicho dhulumu anakiacha hapa hapa.
Anakumbuka jinsi watu maarufu walivyotamba katika enzi zao lakini kwasasa hamna kitu na kwisha kabisa na hakuna anayewakumbuka. Unakuta tukio kubwa linatokea saivi lakini baada ya muda mambo yanaendelea kama kawaida kana kwamba hakujatokea chochote. Anamwangalia mwanadamu anataka aweke historia lakini hakuna cha ziada katika historia hiyo. Wengine walishaweka kabla yako kama ni wasomi au wenye hela wapo walio wahi kuishi kabla yako. Duniani hakuna cha pekee. Sasa muhubiri anavyo tafakari hivi anaona duniani hamna cha pekee na hivyo mwanandamu hana cha kujivunia. Akae tuu kimya aishi maisha yake na muda wake ukifika aondoke.
Roho kama hii ya kiunyenyekevu ilimwingia Mt. Vinsent wa Paulo na kuamua kujihusisha na maskini kwani aliona kabisa duniani ni kukaa kiupole tuu. Sisi tuishi kiupole, tusimuonee yeyote tujishughulishe na wadogo na maskini, maisha ya kudhulumu hayatakufikisha popote.
Katika somo la Injili, tunakutana na mwendelezo wa somo la kwanza, Herodi alimdhulumu Yohane na akawa amebakia na wasiwasi kila wakati. Yeye alikosa upole akaonesha ukatili na akidhania dunia yote ni yake na ama kweli muda sio mrefu alikuja kupoteza kila kitu na ufalme wake wote-afadhali hata kama angeishi kipole. Herode ni kinyume cha mtakatifu Vinsent wa Paulo duniani. Dunia inawahitaji wakina Vinsent wa Paulo, pale tuliopokuwa maherode wa dunia hii hasa kwa kuendekeza dhuluma tuombe msamaha mbele ya Mwenyewezi Mungu
Maoni
Ingia utoe maoni