Alhamisi, Disemba 01, 2016
Alhamisi, Desemba 1, 2016,
Juma la 1 la majilio
Isa. 26:1-6;
Zab 118:1,8-9,19-21,25-27;
Mt 7:21.24-27
NI KITU GHANI KINATUFANYA TUSITIKISIKE?
Leo tunasikia kuhusu wajenzi wawili, mmoja anafanikiwa kwa kujenga nyumba yake juu ya mwamba, na mwingine anashindwa kwa kujenga nyumba yake juu ya mchanga. Mjenzi wa kwanza anaweza kufananishwa na mfuasi wa Kristo ambaye hasikilizi tu neno la Mungu nakuliacha bali analiishi na kulitenda. Kwa upande mwingine, yule anaye sikia maneno ya Kristo, lakini hayaweki katika matendo ni kama yule mjenzi wa pili aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga; kati yetu tumejenga nyumba nzuri kwa mwamba mzuri ili kujilinda wenyewe na tufani mbali mbali, lakini je! Tumeandaa mioyo yetu ili kumpokea Yesu wakati wa Noeli?
Ujumbe wa Injili upo wazi: kama tunataka kushinda mawimbi na dhoruba za maisha na kubaki tukiwa tumesimama imara, tunapaswa kuyaweka maneno ya Yesu ndani kabisa mwa mioyo yetu na kuyaweka katika matendo yetu ya kila siku. Yesu ndiye mwamba imara pekee ambao tunaweza kuwa na tumaini la kweli la kusimamia. Ni msingi wa jinsi tulivyo na yote tunayo tumaini. Ni mwamba ambao Imani yetu imejengwa. Njia pekee ya kumwilisha neno la Mungu katika maisha yetu, ni kusikia neno la Mungu kila wakati katika akili yetu (kusoma neno la Mungu kila wakati). Ni kushibishwa na Neno.
Kipindi hiki cha majilio ni muda ambao tumepewa na kanisa ili tuzame katika msingi wa maisha yetu ya kiroho kwa kusikiliza na kutenda. Tunapo sikiliza, tunapaswa kutenda katika hali ya kumngojea Masiha azaliwe katika mioyo yetu. Kwa njia hii, Noeli itasherekewa katika mioyo yetu ilio simama imara na katika nyumba zetu.
Sala: Bwana, ninaomba maisha yako ulioishi ya kibinadamu yawe msingi wa maisha yangu. Ninaomba maisha yangu yajengwe ndani mwako wewe ambaye ni jiwe la msingi. Yesu, nakuamini. Amina
Maoni
Ingia utoe maoni