Ijumaa. 03 Mei. 2024

Tafakari

Jumanne, Novemba 29, 2016

Jumanne, Novemba 29, 2016,
Juma la I la Majilio

Isa 11:1-10;
Zab 71:1-2,7-8,12-13,17;
Lk 10:21-24.


KUWA MTOTO WA MUNGU!

Somo la kwanza linatufunulia kuhusu habari za Masiha aliye jazwa Roho Mtakatifu na ambaye atakuwa kiongozi mkuu wa duniani na mbinguni kama mtawala wa Amani. Yesu amesha kamilisha mpango wake, lakini sisi tuliotokea kipindi Fulani bado tunapaswa kukubali wokovu wake aliotujalia. Nabii katika somo la kwanza anatangaza wakati mpya, utakao anzishwa na Masiha. Na hapo, alikuwa mfalme aliyetarajiwa, Yesu. Tunamuona yeye akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu akimtukuza Baba yake kwasababu ya ushindi mkubwa dhidi ya muovu shetani. Ushindi huu wanaushinda pia wafuasi wake, wale sabini walifurahi kwasababu walimuona shetani akishindwa (Lk 10: 1-17). Hii ni akili waliopewa wafuasi na Kristo-kwamba Mungu ametukomboa sisi kutoka kwenye dhambi, kifo na maovu yote. Wafuasi wanarudi kutoka katika safari yao ya kwanza ya kimisionari. Wanafurahi “hata shetani anakimbia kwa jina lako Bwana” Yesu anamshukuru Baba yake kwa kuwafunulia mambo haya watu hawa wakawaida, na sio wale walio mashuhuri na werevu wa akili wa dunia hii. Yesu anawaita wafuasi wake “watoto wachanga”.

Je, watoto ni akina nani? Ni wale sabini walio rudi kutoka kutoka katika utume., watu wa akawaida wasio na elimu kubwa, lakini walio msadiki Mungu. Kwahiyo kama tunataka kuelewa vitu vya Ufalme wa Mungu, tunapaswa kuwa wafuasi, wadogo kabisa! Udogo unamaanisha matendo ya Ufalme katika mambo yetu ya kawaida ya maisha. Wafuasi walihisi zawadi hii ya Mungu walio liita jina la Yesu katika mahubiri yao na kuponya. Leo, Yesu anatuita katika uhusiano naye wa karibu na Pia na Baba yake. Anatuita ‘Rafiki”, sio watumwa” kwasababu ametueleza yote kuhusu yeye; na anatuambia tumuite Mungu “Baba yetu” kama yeye alivyokuwa akimwita.
.
Sala: Bwana, nipe moyo wa udogo na mnyenyekevu na imani kama ya mtoto. Nisaidie niweze kukuona wewe kama ulivyo, na kuruhusu uwepo wako duniani uingie katika maisha yangu. Yesu, nakuamini. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni