Ijumaa, Agosti 21, 2020
Ijumaa, Agosti 21, 2020,
Juma la 20 la Mwaka
KUMBUKUMBU YA MT. PIUS X (Papa)
Eze 37: 1-14;
Zab 107: 2-9;
Mt 22: 34-40
AMRI KUU
Injili ya leo inatualika tutafakari njia iliyo kuu ambayo kila mfuasi wa Kristo inapaswa kuwa msingi wake. Upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani. Kwanza kabisa upendo kwa Mungu ni kushuhudia na kukiri upendo wa Mungu kwetu sisi. Sisi ni dhaifu sana na tunashindwa kumpenda Mungu kama inavyotupasa. Lakini ndani ya Yesu tunahisi upendo wa Mungu kwetu. Kwahiyo, kuhisi upendo wa Mungu, licha ya upweke wa mtu mwenyewe inamfanya mtu ampende Mungu kama matokeo ya kuhisi upendo huo. Huu ndio mwanzo wa kumpenda Mungu. Wakati mtoto anavyohisi upendo wa Mama, hafanyi kitu kinyume na Mama. Hii ndio maana ya kumpenda Mungu. Tukihisi upendo wa Mungu hatutafanya mambo kinyume na Mungu, hatujiingiza kwenye dhambi, bali tutafanya yote yenye kumpendeza.
Inamfurahisha Mungu tukiwapenda wengine. Kwahiyo, wakati mtu anampenda Mungu, anaanza kumpenda jirani pia. Je, ni muda ghani upendo wangu juu ya jirani unapokuwa kamilifu? Tunapowapenda ndugu zetu tunakuwa tunatamani na wao kila wakati wawe washiriki kwenye uzima wa milele. Tunakuwa tunatamani na kuomba kwamba waishi maisha yao yote katika neema. Kwahiyo wanakuwa washiriki wa uzima wa milele zawadi tuliopewa na Yesu. Tunakumbuka alichosema Yesu ‘mlicho watendea wadogo hawa mme mtendea yeye’. Tutoke njee ya nafsi zetu, tuweze kukutana na watu waliowahitaji, tuwasaidie kadiri ya uwezo wetu. Huu ndio upendo kwa jirani zetu.
Sala:
Bwana nisaidiye niweze kukupenda wewe ili niweze kuwapenda wengine.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni