Jumatatu, Novemba 28, 2016
Jumatatu, Novemba 28, 2016,
Juma la 1 la Majilio
Isa 2:1-5;
Zab 122:1-9;
Mt 8: 5-11.
UPO TAYARI KUMSHANGAZA YESU?
Leo katika Injili tunamuona Yesu akishangazwa na Imani ya Jemedari. Imani yake ni ya hali ya juu, akiamini, kwamba neno la Yesu linatosha kumponya mtumishi wake hata akiwa mbali. “sema neno tu na mtumishi wangu atapona” (Mt 8:8). Ni Imani iliomsukuma huyu Jemedari, ambaye sio Myahudi, kuamini kabisa kuwa atapona mtumishi wake. Jemedari huyu, akiamini kuhusu nguvu na mamlaka ya Kimungu alionayo Yesu juu ya mambo ya dunia, anatambua dhambi zake mwenyewe na kutostahili kwake Yesu aingie nyumbani kwake. Kwa kutambua madhaifu yetu pia, tunatubu kwa kurudia maneno ya huyu Jemedari kila wakati kabla ya komunyo wakati wa misa.
Kipindi cha majilio ni kipindi cha kuwa makini na kutumaini, tunatambua watu walio karibu na mbali watakao guswa na faraja yetu kwa utayari wetu kwao juu ya mahitaji yao, tunapo peleka mahitaji haya kwa Yesu, je, tunatarajia kwa ujasiri kabisa juu ya upendo wake na huruma yake? Kipindi hiki cha Majilio, tupo tayari, kumshangaza Yesu kwa uongofu wetu wa kweli na matendo mema, matendo ya huruma kwa ajili ya jirani zetu hasa wale waliotengwa na jamii?
Sala: Bwana, nina amini. Nisaidie kwa upungufu wa imani yangu. Nisaidie nione kutokustahi kwangu kila wakati ninapo jiandaa kwa komunyo takatifu. Na kwa kukiri kwa unyenyekevu huo, ninaomba nikaribishe uponyaji wako katika maisha yangu. Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni