Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Agosti 12, 2020

Jumatano, Agosti 12 2020
Juma la 19 la Mwaka


Mt 18:15-20


UJASIRI WA KUPATANA

Ni mara nyingi watu wanapotukosea au wakiishi katika dhambi inayo julikana na wote, huwa tunaingia katika kulaani na kuhukumu. Inakuwa ni rahisi kuwasema. Hili ni jambo la kukosa unyenyekevu na kuruma kwa upande wetu. Huruma na unyenyekevu vitatuongoza kupenda mapatano na kusamehe. Huruma na unyenyekevu vina tatufanya sisi tuone dhambi zao kama sehemu ya kuanza kumpenda zaidi na kumtafutia msamaha licha ya kuhukumu na kulaani.

Huwa unawachukuliaje wale watu waliokukosea, hasa wewe binafsi? Yesu anatutegemea sisi kuweza kumuokoa huyo mdhambi arudi. Unapaswa kutumia muda mwingi kumrudisha katika hali ya kweli. Anza kwa kuongea ninyi kwa ninyi. Jaribu kukaribisha watu wenye hekima na wenye kupenda kufurahi wanapo waona mkifurahi pamoja. Wapo watu wasiopenda kuona watu wakifurahi pamoja. Hata hivyo unapaswa kuwasaidia na wao warudi pamoja katika jumuiya. Jumuiya ya kanisa ina nguvu sana kwani walipo kusanyingika hata watu wawili kwa jina la Mungu, yeye yupo kati yao. Nia kuu ni kuwapeleka kwenye ukweli na kutatua mambo na kufanya mambo yaende tena katika uhusiano mwema. Una waacha tu pale ambapo umefanya kila jitihada lakini wao wakachagua dhambi na kukataa ukweli. Lakini pia kitendo hiki ni kitendo cha upendo kuwasaidia waweze kuona matokeo ya dhambi au maamuzi yao.

Jaribu kutafakari leo, hivi ni nani unapaswa kusameheana naye? Pengine hujafanya tendo lolote kama vile kujishughulisha ili kuongea na muhusika kama hatua ya kwanza. Pengine unaogopa au umeamua kutupilia mbali. Omba kwa ajili ya neema, huruma , unyenyekevu ili uweze kuwakutia wote kwa jinsi Yesu anavyo penda.

Sala:
Bwana, nisaidie mimi niweze kuondokana na maringo yeyote yale yanayo nifanya mimi niwe mbali na msamaha au kupatana. Nisaidie mimi niweze kusamehe hata wakati dhambi niliyo tendewa ni ndogo au kubwa. Ninaomba huruma ya moyo wako ijaze moyo wangu ili niweze kuwa na Amani. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni