Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Julai 29, 2020

Jumatano, 29 Julai, 2020,
Juma la 17 la Mwaka

Kut 24:3-8; au 1Yn 4:7-16
Zab 34:1-10
Yn 11:19-27 au Lk 10:38-48

Kumbukumbu ya Mt. Martha


YESU MGENI WETU WA KWANZA

“Yesu alimpenda Martha na Maria na Lazaro” (Yn 11:5). Maneno haya katika Injili ya Yohane yanatuonesha uhusiano wa pekee waliokuwa nao Yesu na Martha, dada yake na kaka yake. Inaonesha Yesu alikuwa mgeni wao mara kwa mara huko Bethania, kijiji kidogo maili mbili kutoka mji wa Yerusalemu. Tunasoma safari tatu za Yesu kwa Lk 10:38-42. Yn 11:1-53 na Yn 12:1-9.

Safari ya kwanza (Lk 10:38-42) Yesu anamkuta Maria akiwa ameketi chini ya miguu yake akimsikiliza na Martha alikuwa yupo anajishughulisha jikoni. Tunaweza kukubali kwamba wengi wetu tupo kama Martha zaidi kuliko Maria. Maria alichagu upande ulio sawa sawa lakini sisi daima tunachagua sehemu yenye mashaka na masumbuko makubwa. Katika somo la Injili tunamuona Martha akihangaika kwa ajili ya mgeni, alikuwa amesahau kwamba Yesu alikuwa mgeni mkuu na muhimu. Lakini Yesu anapitia katikati ya ukarimu wote na aina yote na kulenga kile kilicho muhimu zaidi. Analenga upendo. Anampongeza Maria kwa kukaa chini na kumsikiliza na anamhimiza Martha afanye vivyo vivyo. Pengine katika maisha yetu tumekuwa na mahangaiko mengi katika maisha yetu na hivyo mwaliko huu wa Yesu tunapaswa kuusikiliza. Tunahitaji muda mwingine wa kuacha kazi na kutafakari na kujisiliza, kuwa katika fikra moja na kuabudu. Tunapaswa kuwa watu wakuwa karibu na Bwana, kumpenda yeye na kulishwa na yeye.

Wakati wa mara ya pili alipo tembelea Yesu (Yn 11), Martha alikuwa akihuzunika kwasababu ya kifo cha Kaka yake. Lakini anaposikia kwamba Yesu amekuja maeneo hayo, anasimama mara moja na kwenda kumlaki Bwana. Anasahau maumivu yake yote na anaenda kukutana na Bwana. Alikuwa mwanamke wa Imani, na anatangaza kwamba “ndio, Bwana. Ninaamini kwamba wewe ni Masiha, Mwana wa Mungu, ajae ulimwenguni”. Na hivyo Yesu anaenda kumfufua kaka yake.

Martha alifanywa upya baada ya Yesu kuwatembelea kwa mara ya kwanza, Yesu alikuwa ndio lengo la maisha yake, anawaacha wote nyumbani na wote wanao omboleza na anakwenda kukutana na Bwana. Sisi nasi tujenge uhusiano huo na Yesu, Mwana wa Mungu. Asiwe tu kwetu mgeni wa kila siku bali tunaomba yeye awe anakuwa daima katika familia yetu.

Sala:
Bwana ninakuomba nikutafute wewe katika ukimya. Ninaomba nikabidhi hofu zangu na woga wangu. Yesu nioshe mimi kwa Neema zako na ninaomba nijiunge tena nawe daima. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni