Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Julai 30, 2020

Alhamisi, Julai 30 2020
Juma la 17 la mwaka wa Kanisa


Yer 18: 1-6;
Zab 145: 2-6;
Mt 13: 47-53


MFINYANZI MTAKATIFU!
Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo basi katika tafakari ya neno la Bwana, tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza. Hapa tunakutana na nabii Yeremia akiifananisha nyumba ya Israeli na udongo wa mfinyanzi ulioko mikononi mwake. Kama mfinyanzi awezavyo kufanya chochote na udongo aushikao mkononi mwake, ndivyo ilivyo kwa wana wa Israeli. Wao ni kama udongo mikononi mwake Mungu. Na hivyo aweza kuwafinyanga kufanya chochote juu yao.
Maneno haya yaonesha nguvu aliyonayo Mungu kwa mwanadamu, na hivyo basi yatubidi kuwa wapole mbele ya Mungu. Tujue kwamba sisi ni udongo, mfinyanzi mikononi mwa Mungu na hivyo tuache kujivuna na kujiamini kupita kiasi.
Tuache na ubabe. Kama tunayo madaraka leo, tujue kwamba kesho kutwa yatakwisha kabisa, yatakuwa ni sifuri tu. Tusijivunie madaraka madogo madogo. Pengine mi kama polisi au wanajeshi tusijivune na kuwa wababe kana kwamba sisi si udongo, mfinyanzi mikononi mwa Mungu. Wasichana tunaojipamba tusiringe kiasi cha kusahau kwamba sisi ni udongo. Watu tunaofanya kazi ofisini tuwe tayari kumpokea kila mmoja. Tuache kuongea vibaya vibaya jamani.tusifanye kana kwambabUlimwengu wote upo mikononi mwetu, sisi ni udongo tu!.
Somo letu la Injili tunakutana na Yesu akiendelea kuelezea namna ufalme wa mbinguni ulivyo. Anatumia mfano wa juya lililotupwa baharini na kukusanya wa kila aina. Na mwishowe mwenye juya atachambua walio wabaya na kuwatupa nje.
Hili linahuzunisha sana hasa endapo kati yetu tutakuwa ni miongoni mwa hawa wadogo ambao tutakuwa hatutakiwi, yaani hatuhitajiki. Hii ni mbaya sana tena kukataliwa na kukanwa kwenye mazingira ambayo wewe mwenyewe ni mgeni! Sasa tutakimbilia kwa nani? Wapi tutakapoomba msaada? Kwani kila mtu ataonekana kuwa mgeni kwetu. Basi tujitahidi jamani, tuishi vizuri, siku hiyo ya mwisho tutakuwa sehemu geni. Sasa, ukitupwa nje, utaishia kuteseka tu kwani hujui utakapopata msaada. Tukitenda matendo mema ni kwamba Yesu atakuwa rafiki yetu na hii itatusaidia kupata wa kukaa nasi kwenye haya mazingira mageni hasa siku hii ya mwisho. Tuwe watu wema.
Tumsifu Yesu Kristo.

Maoni


Ingia utoe maoni