Jumapili, Julai 05, 2020
Jumapili, Julai 5, 2020.
Dominika ya 14 ya Mwaka
Zak 9:9-10;
Zab 4:1-2, 8-11, 13-14;
Rom 8:9, 11-13;
Mt 11: 25-30.
MUNGU ANAJIFUNUA MWENYEWE KWA MASKINI
Jamii ya Wayahudi daima waliongea kuhusu ni nani aliye mkubwa, ambaye anastahili heshima kubwa. Kwa Mungu wa Israeli, ambaye hapinduliwi na miungu ya magharibi, Wagiriki na wa Misri, “ukuu” huu haukukwepeka kwake. Kwa sababu hii Solomon alitangaza na kusema “Yahweh ni mkuu kuliko miungu yote”. (Kut 18:11) na Musa aliwa hakikishia wa Israeli kwamba “Yahweh ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana. Yeye ni Mungu mkuu na wakutisha sana” (Kumb 10:17). Kwa karne iliopita kabla ya Kristo, ujumbe kuhusu ukuu wa Mungu ulienea sana. Alikuwa, Mungu aliye juu, mkuu (Est 8:12). Lakini tazama Kristo anatokea na hali yake, maskini, asiye na kitu, asiye na jeshi la kumlinda, mwenye mama mdogo anaye mjali. Kuanzia hapo ule ukuu ukashushwa. Uwepo wa mwanadamu ni kutafuta uso wa Mungu. Ni yule mtu tu aliye mnyenyekevu anaweza kuuona uso wa Mungu. Masomo yetu yote matatu yanatufunulia kwamba Mungu hujifunua kwa maskni.
Katika somo la kwanza nabii Zakaria anamtangaza Masiha ambaye ni maskini na myenyekevu. Ilikuwa ni muda ambao Israeli hawakuwa tena huru kama taifa, walikuwa wakikandamizwa na kuonewa na mataifa mengine. Watu wa Mungu walikuwa wanategemea kumpata Masiha ambaye atawakomboa kutoka katika utumwa na utawala wa mataifa hayo. Lakini Zakaria anabadilisha mawazo ya utawala wa Kifalme. Mfalme sio yule ambaye anatumikiwa bali yule anaye waweka watu na kuwajali. Wanyonge hawapaswi kujikabidhi kwake, bali yeye hujikabidhi kwa wanyonge ili aweze kuwahudumia. Nguvu zake ndizo watu wanazo ona kuwa ni dhaifu. Yesu anatatimiza unabii huu katika ukamilifu wote pale anapo ingia Yerusalem akiwa amepanda juu ya mwana punda. Kwa ishara hii anaonesha kwamba yeye ni Amani-Mfalme mpendwa aliye tangazwa na nabii Zakaria.
Katika somo la pili Mt. Paulo anaandika kwa Warumi akionesha hali ambayo mtu anapaswa kuwa nayo ili aweze kumpokea Roho wa Mungu. Anasema kwamba Roho huyu anaweza kupokelewa tu na wanyenyekevu na wale maskini wa roho. Mitume wanaeleze hali mpya ambayo wana wabatizwa wamejiingiza. Wanapaswa kufanya kazi ambazo zinaendana na maisha ya Mungu, kwa matokeo ya Roho Mtakatifu. Kama mtu “atachagua kuishi kwa njia ya mwili amechagua kifo”.
Somo la Injili limeanza na Yesu akishangilia: “Baba, Bwana wa mbingu na Nchi, ninakusifu kwani umewaficha mambo haya wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.” Ukitazama wafuasi wa Yesu ni wavuvi wa Galilaya, watoza ushuru, watu wa kawaida, wadhambi, wale wote waliotengwa na jamii. Hawa ndio wale watu waliompokea Masiha na sio wale walio jiona wenye ufahamu mkubwa. Ilikuwa vigumu sana kwa Mafarisayo na waandishi kumkubali Yesu kuwa ni Masiha. Kwanza walimkejeli na kutaka kumtupilia mbali. Ilikuwa ni Maskini waliomkaribisha Yesu na kula pamoja naye na kumsikiliza. Walikuwa na akili kama za watoto wadogo kuweza kupokea hekima ya Mungu na sio hekima ya watu wa ulimwengu. Waliteseka kwa kiu ya haki, wakimsubiri Mungu awainue juu na kuwajaza furaha.
Ukweli wa ndani wa watu wa Israeli ilikuwa kwamba Mungu ni rafiki wa wenye haki tu na wema. Lakini Yesu alienda kuwa toa wale ambao tumewatupa mbali. Aliwatazama wale ambao hakuna mtu wa kuwatazama, wanao onekana wadhambi wa mwisho na wasiofaa (Mt 11:19) na makahaba (Mt 21:31) kwani aliwapenda sana aweze kuwaokoa. Kwani Yesu anasema “hakuna amjuae Mwana ila Baba na wala hamna amjuae Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia”. Neno “kumjua” katika Biblia halimanishi mlikutana au kuwasilana na mtu muda Fulani, ila “kuwa na uzoefu kamili kabisa kuhusu huyo mtu”. Linatumika pia kuonesha kuwa na uhusiano wa ndani kati ya mke na muwe (rej. Lk 1:34). Akili kamili kuhusu Baba inawezekana tu kwa njia ya Mwana. Lakini anaweza kumfumbulia yeyote ampendae kadiri ya mapenzi yake. Ni nani atastahili kupokea ufunuo huu? Wale wadogo kwa hakika. Waandishi na Marabi walijifunza kila nyanja zote za sheria walijiona wao ndio wenye elimu yote kuhusu Mungu. Walibaki wakisema kwamba wana uwezo wakutambua lililo jema. Walijionesha wenyewe kuwa kama mwanga kwa wale walio katika giza, kama walimu kwa wale wajinga, na mabwana wa wale walio wadogo (Rum 2:18-20). Jinsi walivyo jiweka na kujiona wenye hekima na akili ndivyo walivyo jifungia hekima ya Mungu na utambuzi juu yao.
Mafarisayo na waadishi walikuwa wametengeza dini ya hali ya ajabu, kutengeneza sheria ambazo haikuwezekana kuziishi. “Waliwatwisha watu mizigo ambayo wao wenyewe hawakuigusa kwa vidole vyao” (Lk 11:46). Kwa njia hiyo maskini hawakujisikia tu wanyonge bali walijiona hawafai mbele ya Mungu na hata katika ulimwengu ujao. Kwa maskini na wale walio tengwa Yesu alitangaza uhuru na kuweka dini ya kweli. Aliwaambia wapokee sheria yake ambayo ni laini ambayo inaweza kufupishwa kwa neno la Upendo. Nira yake laini. Kwanza kabisa nira ni yake, si kwasababu anaiweka tu, bali yeye ameiishi kwanza. Nira yake ni tamu kwasababu ni kwa wale tu wanaweza kumpokea wanaweza kufurahia hekima yake na Amani. Mwisho, anatualika tujifunze kutoka kwake, kwani “mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo”. Yesu anajionesha kama mpole na mnyenyekevu. Haya ni maneno ambayo tunayapata kutoka katika zile heri. Hayaoneshi woga, bali yanaonesha unyenyekevu kwa wale wote wanaoteseka kwa ajili yake lakini hawajibu kwa tukano.
Sehemu ya Injili ya leo ni sababu ya tafakari binafsi na tafakari ya jumuiya. Kuishi kwa uyenyekevu ili Mungu aweze kujifunua kwetu kwa ukweli ambao anatamani kutufunulia. Tafuta kukuwa katika unyenyekevu ili Mungu aendelee kujifunua kwako. Kazana daima kuwa mtoto wa Mungu na utakuwa mwenye hekima zaidi na zaidi kuliko jinsi ambavyo ungeweza kuwa kwa nafsi yako mwenyewe.
Sala:
Bwana mpendwa, nisaidie mimi niweze kuwa mnyenyekevu na kuwa na Imani ndani yako, na kwa njia ya Imani hii, niweze kufahamu mafumbo matakatifu unayo penda kunifunulia mimi. Nipe hekima na akili Bwana wangu, zaidi ya kile ambacho ningeweza kupata kwa nafsi yangu mwenyewe. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni