Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Juni 21, 2020

Jumapili, Juni 21, 2020.
Dominika ya 12 ya Mwaka


Yer 20: 10-13;
Zab 68: 8-10, 14, 17, 33-35;
Rom 5: 12-15;
Mt 10: 26-33.


YESU YUPO PAMOJA NASI KUTUOKOA!

Kabla ya kuingia katika barabara kuu ukitokea mitaani, lazima kuwa makini na mwangalifu kwa kuangalia pia alama zilizo wekwa. Ni vizuri kuangalia kama tunafuata gari jingine au kuna mtu barabarani. Hivyo hivyo, wafuasi wa Yesu wanapaswa kuwa makini katika kutembea kinyume na mapigo ya dunia. Kama wakichagua njia ya kujikatalia, kuwapenda watu, kusamehe, uaminifu, wata waona watu wakitembea mwelekeo mwingine. Na watatambua kuwa na kuchukua tahadhari kwamba haijalishi nakuwa mwaminifu namna ghani, migongano haikwepeki. Watakuwa tu watu wakuteseka, kuonekana kama waliopoteza mwelekeo, wavunjifu wa sheria zinazo kubalika na wote. Hili pia laweza kuwafanya wakristo kujisikia kwamba wamechagua njia isiyo sahihi.

Katika somo la kwanza tunakutana na Yeremia aliyeishi katika kipindi katika historia ya mwenendo usio kuwa mzuri wa watu wake. Jeshi la Nebukadneza limeizunguka Yerusalemu na kuichukua mateka. Mfalme na majeshi yake wamefanya maamuzi yasio kuwa sahihi ya kuleta maangamizi. Badala ya viongozi wa dini kutambua yanayo wapata watu, wanamsifia Mfalme na jeshi lake. Katika hali hii ngumu, Yeremia kijana mdogo, mwenye aibu, na mtu wa amani anaitwa na Mungu kufanya utume hatarishi juu ya “Mfalme wa Yuda na viongozi wake, makuhani wake na watu wote katika nchi”. Ana imarishwa na Bwana kwa maneno haya “watapigana nawe lakini hawata kushinda, kwani nipo nawe kukuokoa” (Yer 1:17-19). Yeremia anakutana na upinzani. Maadui wa Yeremia hawaja jifunga tu katika makundi bala wanamtafuta ili wamtundike na kumuua. Yeremia anaona utume wake umeshindwa, anajisikia kukataliwa na watu wake na watu wote. Anakata tamaa, na kujiuliza kama kweli wito wake pengine haukuwa wa kweli. Anaeleza hisia zake kwa Mungu. Sala yake alioifanya kwa mkazo, lakini katika uaminifu, inaleta matokeo kwake ya ukweli wa uamini fu wa Mungu. Ujasiri wake na matumaini yake yana amka tena. Anatangaza: “Yahweh Bwana wa majeshi yupo nami” (mstari. 11). Ana ujasiri na uhakika kwamba Mungu, Mungu atamshindia, anafanya ukweli utawale na kumfanya mwenye kutetea haki kungara.

Katika somo la pili kutoka barua kwa Warumi, Paulo anamlinganisha Adamu na Yesu: analinganisha matokeo ya dhambi ya mtu wa kwanza na matokeo ya ukombozi ulioletwa na Kristo. Tangu awali mwanadamu alitenda dhambi, kwa kufuata mfano wa Adamu aliyekosa utii na kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu, lakini, Yesu alifanya kinyume chake. Yeye ni mtii kwa Baba, ametimiza mapenzi yake mpaka kufa. Matokeo ya dhambi ya Adamu ni kifo. Neema inayo patika kwa utii wa Kristo, ni mkuu sana. Kwa njia ya Kristo, Mungu amewapa uhai wote.

Katika Injili ya Mathayo iliyo andikwa kipindi cha Mfalme Domitian wa Kirumi, aliye amuru kuabudiwa kama Mungu. Wakristo hawakuweza kumpa mfalme sifa za Mungu. Kwa njia hiyo, matatizo yalianza, kupigwa, kutengwa, mali zao kuchukuliwa yalianza juu yao. Walio wengi hawakuweza kuvumilia unyanyasaji wa namna hii. Walikuwa katika hali ngumu ya kufanya uamuzi. Hivyo, ili kuwafariji wakristo wa jamii yake, Mathayo ana andika maneno hayo ya Yesu, ya kihistoria, ambayo aliyaweka katika Injili, maneno ya Yesu kuhusu kupatwa na magumu na mateso kwa wafuasi wake. Kwa Wakristo mateso sio ajali; haya kwepeki: “wale wote wanaotaka kumtumikia Mungu kwa njia ya Kristo, watateseka”. (2 Tim 3:12).


Katika Injili ya Leo, Yesu anasisitiza mara tatu “msiogope!” na kila wakati ameongeza motisha ili kuonesha msisitizo wa ujumbe wake. Yesu ana tuhakikishia kwamba licha ya magumu na mateso, Injili itaenea ulimwenguni na kuubadilisha. Yesu anatuita pia tutafakari: ni madhara ghani adui wa Injili anaweza kuleta? Kusingiziwa, kuhukumiwa bila haki, kupigwa, kuchukua mali, kuuwawa! Ndio, lakini hamna zaidi! Hakuna vita vyenye uwezo wakuweza kuchukua thamani ya uzima: uzima aliotoa Mungu hakuna anaye weza kuuchukua. Lakini kuna mtu-Yesu anaendelea-ambaye anapaswa kuogopwa. Ni “yule ambaye ana nguvu ya kuangamiza mwili na roho kwa pamoja”. Hali hii sio hali ya nje, bali niuovu ambao tangu kuzaliwa, tunauchukua ndani mwetu. Hii ni msukumo mbaya unao tuongoza kwenye njia tofauti na njia ya Kristo. Hivyo tunapaswa pia kujiogopa sisi wenyewe na hofu yetu. Yesu anatuita kutegemea nguvu ya Mungu. Anatupa uhakika kwamba Mungu atatambua uzuri wetu kama tutakuwa jasiri na kubaki waaminifu.

Sala:
Baba wa Mbinguni, ninakushukuru kwa upendo wako katika maisha yangu. Ninakushukuru kwa kuniita mimi na kunibadili ili niweze pia kubadili ulimwengu. Nisaidie mimi nitegemee upendo wako na kujikabidhi kwako. Katika nyakati za mateso, kuwa nguvu yangu na tumaini. Ninawaombea pia wakristo wote wanao onewa ulimwenguni, ili waweze kuvumilia mpaka mwisho. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni