Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Mei 10, 2020

Jumapili, Mei 10 2020.
Juma la 5 la Pasaka
Mdo: 6:1-7
1 Pet 2:4-9
Yn:14:1-12

Mungu ni nani? Nani amemwona Mungu? Nani anaweza kuelezea kuhusu Mungu?
Mkristu humzungumzia Mungu, kutokana na uelewa wake. Mwisilam humzungumzia Mungu, kutokana na uelewa wake. Na Myahudi hivyo hivyo. Kwa hiyo, kila dini humwangalia Mungu, kulingana na uelewa wake. Kwa sababu hiyo basi, kila mtu ana mawazo tofauti kuhusu Mungu. Hakuna ulinganifu kabisa. Kwa hiyo, ninaweza kusema nimechanganikiwa, kuhusu nini cha kukubali na nini cha kuamini?
Masomo yetu ya leo, yanatueleza kuhusu hilo. Yanatupa malezo, ambayo yana manufaa kwetu. Katika Injili ya leo, tunaona Yesu, akielezea ukweli kuhusu Mungu, kwa sababu yeye anatoka kwa Mungu na anaenda kwa Mungu. Atamchukua kila mmoja wetu kwa Mungu. Kwa sababu hataki hata mmoja wetu apotee. Na anathibitisha hilo kwa kusema yeye ni Njia ya kwenda kwa Baba, na hakuna njia nyingine tofauti na Yeye. Kwa sababu Yeye anamjua Baba.
Yeye ni Ukweli, kwa sababu amejifunza kila kitu kutoka kwa Baba, kwa hiyo anaongea ukweli. Na Yeye ni Uzima, kwa sababu yote aliyoyozungumza, na kuyafanya ni yale yanayoyeeleza ubora wa maisha yetu. Na anasema, ye yote aliyemwona yeye, kumhisi Yeye, na kukutana naye amemwona Baba. Kwa hiyo Yesu anajitambulisha kuwa ni Mungu, kwa hiyo yeye ni Mungu.
Kuna ye yote anaweza kusema anamfahamu Mungu kama alivyo Yesu ambaye ni kiongozi wa wakristu? Kuna ye yote aliyesawa na Mungu, kama alivyo Yesu? Kila mtu anazungumza kuhusu Mungu. Lakini Yesu hakuzungumza juu



ya Mungu tu, bali pia alizungumza kwamba Yeye na Mungu ni mmoja. Ye yote aliyeniona mimi, amemwona Baba.
Uthibitisho huu wa Yesu, unaonekana katika Injili, katika matukio mbalimbali na kwa maneno tofauti.
Kwa maana hiyo basi, sisi wakatoliki hatuwezi kusema kwamba tunamjua Mungu kuliko dini nyingine? Lakini katika hali halisi ni kweli? Kwa sababu tumeshindwa kumfanya Yesu Njia, Ukweli na Uzima.
Katika somo la kwanza, tumesikia kazi za ajabu za Mungu. Idadi ya wafuasi inaendelea kuongezeaka kwa sababu ya neno la Mungu, linalohubiriwa kwao na mitume. Kutokana na hali ya ubinadamu, ya uelewaji kulitokea matatizo, ambayo yalitatuliwa kirahisi na mitume, ambao walikuwa wanaongozwa na Roho wake Mtakatifu. Pia tumeona ni jinsi gain, mitume walivyofanya kazi kwa bidii ingawa walikutana na matatizo yote hayo. Hii ni kwa sababu, waliuona na kuuhisi uwepo wa Yesu kati yao.
Katika somo la pili, tunaelezwa kwa ubatizo wetu kila mmoja wetu, ni jiwe la uzima katika kanisa, ambalo Mungu huishi, watu wa taifa teule la Yesu, na taifa takatifu, na watu ambao Mungu anajivunia kuwa wake. Ni aina gani ya upendeleo kwetu sisi. Je, kwa nini tunakuwa wagumu hivyo? Tuna matatizo gani?
Tuna habari hizo nzuri za upendeleo, katika masomo yetu ya leo, kwamba Yesu, Mwana wa Mungu, amekuja duniani, na kutufundisha kuhusu Baba yetu wa mbinguni. Ni habari njema Yesu, aliishi kati yetu katika maumbo ya mwili na damu kama tulivyo. Ni habari njema, kwamba Yesu anaendelea kuishi, kati yetu leo katika fumbo la mwili, ambalo ni kanisa lake hapa duniani. Hii ni habari njema, na ndiyo maana tunaadhimisha Ekaristi takatifu leo na siku zote.

Maoni


Ingia utoe maoni