Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Mei 06, 2020

Jumatano, Mei 6, 2020.
Juma la 4 la Pasaka


Mdo 12:24-13:5;
Zab 67:2-3,5-6,8 (K. 4);
Yn 12:44-50.


YESU, MWANGA KWA ULIMWENGU!

Kumfahamu Yesu ni kumfahamu Baba pia. Ukweli ni kwamba uwepo wa Baba umefunikwa kama Umungu wa Kristo ulivyo funikwa. Ingawaje hatuna uzoefu wa kumuona Yesu akitembea kama wale wafuasi wa kwanza walivyo muona, tunakutana na ukweli huo huo katika Ekaristi Takatifu. Wakati tunapo ingia kanisani na kupiga goti kuelekea Tabernakulo, ni vizuri kuwa na uelewa na kufahamu kuwa tupo mbele ya uwepo wa Mungu Mwana. Na kwa njia hiyo tupo pia mbele ya uwepo wa Mungu Baba! Uwepo wao ni wazi na hakika. Ni kwasabau tu wamefichwa kutoka katika milango yetu mitano ya fahamu.

Katika Injili, Yesu anakuja kama nuru ili tusiwe tena kwenye giza. Anakuja kwa lengo hili: tumuamini yeye na kuwa na ukweli na uzima. Zaburi ya 27 mstari wa 1, unasema “Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu”. Kama ilivyo mwanga wa kawaida hufunua kile kilicho fichwa kwanye giza, vivyo hivyo Neno la Mungu huleta nuru ili tuweze kutambuaa ukweli ulio fichika ndani ya Ufalme wa Mungu. Kama nuru, huleta furaha na uzima kwa wengine. Inafanya mbegu ya imani ikue ndani yetu, ili tuweze kushiriki furaha ya Mungu na uzima na wengine. Sisi mara nyingi tunachagua kubaki kaburini kama Mafarisayo bila kufufuka. Lakini Yesu ni mlango wa uzima wa milele. Kwani Yesu ni uzima na ufufuo na wote wale wanao mwamini watakuwa na uzima wa milele.

Sala:
Bwana, nisaidie niweze kukuelewa wewe na kukupenda wewe na katika uhusiano huo niweze kumfahamu na kumpenda Baba na Roho Mtakatifu. Bwana, ninaomba wewe uwe mwanga ambapo kwa njia yako niweze kukuona wewe na ulimwengu. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni