Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Aprili 10, 2020

Ijumaa, Aprili 10. 2020
Juma Kuu

IJUMAA KUU

Isa 52:13-53;
Zab 31:2,6,12-13,15-17,25
Ebr 4:14-16, 5:7-9;
Yn 18:1 - 19:42

MTAZAMENI MTU!

Wakati wa vita vya pili Mt. Maksimiliano Kolbe alifungwa kwenye kambi kubwa. Kule kumwokoa mwenzake mfungwa, Maksimiliano Kolbe anasogea mbele kufa kwa ajili yake. Hapa tunaona kujitolea kwa ajili ya wengine.
Wakati wa vita kuwaokoa wanajeshi waliojeruhiwa na kuwapeleka mahali pausalama wengi wanachukua hatua bila kujali juu ya maisha yao. Hapa tena tunaona ushujaa kweli.
Leo tunakumbuka mtu mwenye ushujaa, ambaye ni Yesu Kristo alijeruhiwa, alikufa na alitoa uhai wake kwa ajili yetu sisi, kutuokoa. Kifo cha mtu mmoja ambaye kifo cha Bwana Yesu kilituokoa sisi sote. Leo Mama Kanisa Takatifu, kwa namna ya pekee anafanya ukumbusho wa kifo cha Yesu Kristo na anatukumbusha sisi sote kuwa waaminifu zaidi kuheshimu jina lake na kutumikia.
Yesu alipohangaika msalabani, wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, “aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini” (Mt. 27: 41-43). Yesu aliweza, lakini alikuwa na mpango mkubwa kwa kuokoa siyo kwa wachache tu, bali kwa wanadamu
wote. Ndiyo maana yeye alikuwa tayari kunywa kikombe cha utii na kuyafanya mapenzi ya Baba yake, “ walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe” ( Mt. 26:39). Huo ni upendo wake mkubwa kwa ajili ya kila mmoja wetu, ili tusipotee lakini ili tuweze kuishi daima na milele. Kitu ambacho alisema, yeye alionyesha kwa kitendo katika maisha yake – “ hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yn. 15:13). Yesu alimpenda kila mmoja wetu kama marafiki zake. Je, siyo zamu yetu kumpenda Yesu? Je, kweli tunampenda?
Kuna wimbo uliandikwa na shahiri moja unaitwa, “ Four Initials On The Tree”, maana yake, herufi nne juu ya mti. Hadithi ya wimbo huu ni, mtu mmoja akaja baada ya miaka kadha akarudi kijijini kwake na akatembelea pembeni ya shule ya sekondari ya zamani akajifunza. Akaona mti ule pale ambapo yeye na mchumba wake miaka iliyopita walichora herufi zao. Kitu kimeingilia katika uhusiano wao na walitengana lakini herufi zao zilibaki palepale. Kitu ambacho kilibaki cha upendo wao ni herufi nne tu juu ya mti ule.
Miaka iliyopita kwa wengine ni mengi, na kwa badhi yetu ni michache, sisi tulimpenda Yesu Kristo na siku moja tulibatizwa, na tulichora herufi zetu juu ya mioyo yetu. Wakati miaka inapita wangapi tunabaki waaminifu kwa ahadi ya upendo? Ijumaa Kuu, yaani leo, wakristu wengi wanahudhuria ibada, labda wanakumbuka upendo wa kwanza kabisa na Yesu Kristo. Mwanzo wa upendo, yaani mwanzo wa maisha ya kikristu, tuna kuwa na hamu ya kupata ubatizo mapema. Wakati siku zinapita mahuduhurio yanaanza kuwa hafifu, wivu, yanarudi nyuma zaidi na zaidi. Tunasahahu kuhusu ahadi zetu kwa kumpenda Yesu daima. Lakini tukumbuke, herufi nne zimebaki juu ya mti hata siku ya leo, JNRJ: yaani Jesus Nazerenus Rex Judaeorum, maana yake, Yesu wa Nazereti, Mfalme wa wayahudi. Kwetu sisi Yesu alikufa kutimiza ahadi ya upendo isiyo kifane. Kama upendo wetu umekuwa hafifu, tunaweza kuchochea tena. Kwa sababu upendo wa kweli ni wa milele. Tusikie! Labda anatuambia kila mmoja wetu, “ napenda kurekebisha uhusiano wa zamani na wewe siku ya leo, sasa hivi”- imesahihi na Bwana Yesu,

Maoni


Ingia utoe maoni