Ijumaa. 22 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Novemba 16, 2016

Jumatano, Novemba 16, 2016,
Juma la 33 la Mwaka wa Kanisa

Ufu 4:1-11
Zab 150: 1-6
Lk 19:11-28


KUWA WAZALISHAJI KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU!

Mfano wa leo kutoka katika Injili, wakati Mfalme alivyorudi, alihitaji hesabu kutoka kwa kila mtumishi. Kwa njia hii kila mmoja wetu atatoa hesabu ya jinsi tulivyo tumia vizuri talanta na vipiji tulivyopewa na Mungu. Kati ya Wayahudi waliokuwa katika mstari wa Mafarisayo, wao walidhania Mungu kuwa hakimu mkali aliyewatenda kadiri ya faida waliopata kwa kushika sheria. Hali hii iliwajengea watu hofu na wakashindwa kukuwa. Na zaidi sana, iliwafungia hata wao wenyewe kushindwa kufungua mioyo na kukubali hali mpya ya kukutana na Mungu alioleta Bwana wetu Yesu Kristo. Je, wewe na mimi tukoje? Tumetumiaje, au tunatumiaje vipaji alivyotupa Mungu? Je, tutakana uaminifu wake kwetu?

Sala: Baba, nakushukuru kwa kuni amini mimi na kunipa vipaji na nafasi, yote yaliotoka katika mikono yako. Nisaidie mimi nijifunze kuwa mzalishaji wa kweli kwa ajili ya ufalme wako. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni