Alhamisi, Aprili 09, 2020
Alhamisi, Aprili 9.2020
Juma Kuu
ALHAMISI KUU
Kut 12: 1-8,11-14;
Zab116: 12-13,15-18;
1 Kor: 11:23-26;
Yn 13: 1-15
FANYENI HIVI KWA KUNIKUMBUKA MIMI!
Kuwapa zawadi ni kama kawaida mahali popote. Wakati sherehe ya ndoa, upadrisho, sikukuu ya kuzaliwa n.k. sisi tunawapa zawadi, vitu vya kawaida. Lakini wakati tunaaga, sisi tunawapa zawadi ya pekee kama kumbukumbu. Zawadi hizo tunaheshimu sana, mara nyingi zawadi hizo tunaweka sehemu ya pekee. Tunaziangalia na tunamkumbuka, yule ambaye alitupa na tunasikia uwepo wake.
Tukio kubwa kama hilo tunasherekea siku hii ya leo. Yesu aliwapenda wanadamu kwa upendo mkubwa, hata mimi na wewe, kwa hiyo kabla ya kifo chake Yesu alitupa zawadi ya thamani, kama alama ya upendo wake, ili tuziheshimu kwa upendo mkubwa. Zawadi hizo ni zawadi gani?
Leo ni siku malumu katika maisha ya kikristu. Tunakumbuka matukio matatu au zawadi tatu ambazo zilizotokea siku ya pekee ya leo. Kwanza kabisa kuweka Ekaristi Takatifu. Yesu alitwaa mkate na kikombe, alisema, ‘twaeni mle; huu ndio mwili wangu…Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu…’(Mt.26: 26-28) tangu saa ile Yesu amekuwa Mwana Kondoo wa Pasaka, sadaka kwa Mungu, Mwana Kondoo ambaye aondoaye dhambi za dunia. Kwa hiyo Ekaristi ni ishara za kifo na ufufuko wa Yesu.
Yesu alituaga na kutupatia Ekaristi, kama zawadi ya kwanza kwetu sisi. Kwa kushiriki mwili na damu kama chakula cha kiroho, ili tuwe na nguvu imara na kushinda maovu ya dunia, tuwe na uhodari wa kutembea njia nyembamba ya wokovu, tuwe na ukarimu zaidi kuwapenda wenzetu daima. Mwaka huu ni mwaka wa Ekaristi. Kiasi gani tunaziheshimu zawadi ambayo Yesu alitupatia? Je, tunashiriki chakula cha Bwana? Na tunaadhimisha Ekaristi mara kwa mara?
Ebu tuangalie zawadi ya pili. Yesu aliweka Daraja Takatifu la Upadre. “ Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi”, kwa maneno haya Yesu aliwaagiza wanafunzi wake kuendelea kuadhimisha sadaka takatifu ya Ekaristi, kuumega mkate na kuwalisha waumini, ili waweze kusafiri kuelekea uzima wa milele.
Kwa hiyo zawadi ya pili ya Yesu ni Upadrisho. Kwa njia ya zawadi hii Yesu anapenda kuwalisha kwa njia ya huduma ya mapadre. Kiasi gani tunawapenda mapadre wetu? Je, tunawaombea hawa? Kiasi gani tunatambua huduma zao?
Zawadi ya tatu ni Amri ya Upendo. Yesu aliwakaribia kuwa tayari kuwasaidia wote. “Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielekezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende viviyo hivyo”(Yn.13: 14&15). Hii ni Amri ya Upendo na Kutumikia. Haya ndiyo tutaona baada ya mahubiri, kuwaosha miguu ya kumi na wawili kunatueleza jinsi Yesu alivyofanya. Siyo maana yake kwamba tunatakiwa kuwaosha miguu, siyo kwamba kuwaosha kwa maji, lakini ina maana kuwa tayari kuwatumikia hasa wale wanaotuhitaji. Je, tuko tayari kuwatumikia?
Kwa hiyo NZW, siku ya leo ni siku kubwa kwa Mama Kanisa, kuziheshimu zawadi hizo za Bwana Yesu, na kukumbuka au kuadhimisha, na kusikia upendo na uwepo wa Bwana Yesu Kristo hapa sasa hivi. Wakati tunaadhimisha siku ya pekee ya leo, tufanye thathmini kiasi gani kwa kweli tunapokumbuka zawadi hizo, kiasi gani tunatambua uwepo wa Bwana Yesu, na kiasi gani tunaonyesha upendo na tunamshukuru yeye? Tumwahidi leo sasa hivi tutaziheshimu zawadi hizo kwa upendo mkubwa.
Maoni
Ingia utoe maoni