Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Jumamosi, Julai 02, 2016

Jumamosi, Julai 2, 2016,
Juma la 13 la Mwaka wa Kanisa


Amo 9:11-15;
Zab 84:9-14;
Mt 9:14-17

yesu, dira ya furaha

Dira ni kifaa kinachotumika na watu kama wanajeshi, nahodha nk. Masomo ya leo ni kama dira, yana tufunulia Umungu wa kweli ndani ya Yesu. Kama dira inavyo muongoza nahodha ili kufika mwisho wa safari yake. Pia Yesu ni dira yetu anatuongoza ili tufike kwenye furaha ya milele. Lakini furaha hii haipatikani hivi hivi, ni lazima kupitia mawimbi mbali mbali kama nahodha anapopitia njia mbali mbali na sehemu asioijua ili kufikia lengo lake, Yesu ni nahodha pekee aliyekuwa na hakika ya ushindi wake, mateso, kifo na ufufuko. Hata njia yetu itakuwa hivyo hivyo. Pili maisha yetu ni kama kioo kinacho tuonesha jinsi tulivyo. Lakini tunapomchukua Yesu, kama divai mpya na mawazo mapya na mtazamo mpya wa ukweli, yeye anakuwa kioo chetu cha kumulika maisha yetu nakutambua ukweli halisi ya kuwa tunapaswa kuwa tofauti zaidi na jinsi tulivyo sasa. Maisha ya zamani tuliyo jijengea yenye sheria ngumu na tena nyingine zenye ubinafsi na chovu au mambo mengine yanayopingana na upendo wa Yesu yanapaswa yaondolewe na kuwa kiumbe kipya na kuweka mambo mapya yaliosimikwa katika upendo wa Yesu.

Kwahiyo kuna ulazima wa kubadili maisha yetu. Kwakumuweka Yesu kama kioo mbele yetu ili amulike maisha yetu. Hapo tutaona nafsi yetu ilivyo tofauti na nafsi ya Yesu ambaye sisi wote tumeitwa kuishi maisha yake. Maisha yangu yanapaswa yawe kama maisha ya Yesu, kama nashindwa kuishi kama Yesu alivyo basi napaswa kubadili mienendo yangu. Tutafute ukweli kuhusu nafsi zetu zaidi na tuondoe ile hali yakutaka kujua tuu ukweli kuhusu maisha yawengine na kuficha yetu. Tunapoteza muda mno kutaka kujua nafsi za wengine, tuanze na nafsi zetu na moja kwa moja mafanikio yataonekana na wengine. Tuombee neema ya Mungu ituongoze ili tuweze kubadili maisha yetu kwanza katika kweli ya Yesu kabla hatuja thubutu kuwarekebisha wengine.

Sala: Nitafurahi katika Bwana, nitamtukuza Mungu mwokozi wangu. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni