Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Februari 20, 2020

Alhamisi, Februari 20, 2020,
Juma la 6 la Mwaka wa Kanisa

Mk 8: 27-33.


UHURU KUTOKA KATIKA HOFU YA MSALABA!

Yesu alianza kufundisha Mitume kwamba bado kitambo kidogo atateswa sana, kukataliwa na kuuwawa. Hili ni lazima lilikuwa gumu kukubali na kueleweka kwa Mitume. Kwanza kabisa, ni lazima walikuwa wamehisi ugumu na huzuni tunayo pata pale tunapo kumbana na habari mbaya. Tunaweza kuanza na kukataa, baadae kupata hasira, kuanza kutafuta suluhisho, kuchanganyikiwa, n.k. Kupitia hatua za huzuni na kukubali ni kawaida na hili ndilo Petro lililo mpata.

Petro anampeleka Yesu pembeni na kumweleza. Inaonekana ilikuwa imejikita kwenye hofu aliokuwa nayo Petro moyoni. Katika hali yake ya ndani ya kukazana kujaribu kuelewa yale aliokuwa anawafunulia Yesu, petro anajaribu kuweka kipingamizi. Katika Injili ya Mathayo tunasikia maneno halisi ya Petro, “Mungu anakataza, Bwana, hakuna kitu kama hicho kitakacho kupata” (Mt. 16:22). Maneno ya Petro kwa hakika yalikuwa maneno ya kuonekana kumjali Yesu, lakini ni vizuri kutambua kuwa, haina maana kwamba Petro kumjali Yesu, maneno yake yalikuwa ya msaada.

Kadiri ya Injili inavyo endelea, Yesu anamkataza Petro kwa ukali kabisa, lakini anafanya haya kwa upendo kwasababu alitaka Petro aondokane na hofu na kuchanganyikiwa kwake. Inatambulika kuwa Petro alikuwa ana hofu juu ya utabiri wa kuwepo kwa msalaba. Inaeleweka mmoja wetu anapo patwa na hofu kwasababu ya matatizo falani au msalaba fulani. Cha muhimu hapa tunacho ambiwa ni kwamba Yesu hapendi sisi tubaki katika hofu. Hataki tukimbie misalaba yetu tuliopewa kwasababu ya udhaifu wa kibinadamu. Badala yake, anataka tumgeukie yeye na kuanza kufikiri kama yeye anavyo fikiri, kutenda kama anavyotenda, na kukabiliana na matatizo kama yeye alivyo kabiliana nayo kama alivyo fanya kwa kupitia msalaba. Tusikubali maumivu ya kubeba msalaba yatufanye tukimbie msalaba. Mfano huenda kumtunza ndugu yako mgonjwa yaweza kuonekana msalaba kwa muda mrefu, Yesu anatutaka tubebe mpaka mwisho kwani zawadi yetu ipo ndani ya msalaba huo. Tuombe ili tuweze kuwa na ujasiri wa kubeba misalaba yetu na pia tufungue mioyo yetu kuelekea kwenye upendo wa Yesu, ili aweze kutuondolea hofu yote katika kubeba misalaba yetu.

Sala:
Bwana, ninatambua kuwa wewe ulikabili kwa ujasiri na bila hofu mateso ya msalaba kwa sadaka yako takatifu msalabani. Unapo nialika kufuata nyayo zako, ninaona pia hofu inaweza kunikumba kama ilivyo mkumba Petro. Tafadhali Bwana nipe ujasiri ninapo kumbana na nyakati hizi na pia nipe neema ninayo hitaji niweze kusema “ndio” kwa yote unayotaka nifanye. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni