Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Februari 07, 2020

Ijumaa, Februari 7, 2020,
Juma la 4 la Mwaka wa Kanisa
1 mfa 3:4-13
Mk 6: 14-29.


CHAGUA KULINDA MAISHA!

Leo tunaona mwisho na unyong'onyevu wa mwenye haki na asiyeogopa nabii wa kweli Yohani Mbatizaji katika mikono ya mtawala dhalimu, aliye jazwa na tamaa, na picha ya utukufu dhalimu wa uongo wa hadhi na heshima! Herode alifanya makosa makubwa matatu, ambayo mtawala mwenye kuwajibika hapaswi kufanya hivyo. Kwanza, yeye alionesha mfano mbaya, kwa kumuoa mke wa nduguye. Pili, yeye alifanya ahadi ya bila kufikiri kwa yule msichana aliyecheza. Tatu, alihofu watu watasema nini na kujaribu kuokoa heshima yake ya uongo, aliamuru mauaji ya mtu mwenye haki asiye na hatiya. Yohane Mbatizaji.

Hakuna mtu mwenye haki ya kucheza na maisha ya mtu mwingine, iwe katika gereza au katika mitaa au akiwa tumboni. Na waliopo katika madaraka, wana wajibu wa kulinda maisha, na wanalazimika kufikiri mara mbili na kufanya hakika kwamba maisha hayapo hatarini.
Tutafakari leo, kuhusu hali zetu za kila siku za maisha. Je, unapatwa na hasira na kujifanya kuielekeza kwa wengine ambao hawastahili? Tutafakari juu ya tabia hizi na tuangalie kwa undani chanzo chake. Kama ukiona chanzo cha tabia hii ambayo sio nzuri pengine ni kwasababu ya dhambi yako mwenyewe ya maisha yako, tubu kwa hakika na kuimaliza ili Bwana wetu akuweke huru kutoka katika malipo yake.

Mara moja nyuki, ambaye mwenendo wake ulikuwa mzuri na kama asali anayofanya, alikwenda kwa Mungu na kumuomba mafanikio akisema. "Naomba ninapo muuma mtu afe hapo hapo." Mungu akashtuka. Mafanikio mara moja yakabadilishwa na kuwa laana. "Mungu akasema ni sawa. Lakini yule atakayeuma ndiye atakayekufa sio yule atakayeumwa” "Mungu anapenda maisha ya endelee, sio yaharibiwe.

Sala:
Bwana, natubu dhambi zangu zote. Ninasali ili niweze kuziona dhambi zangu kwa uaminifu kabisa na kwa kweli. Ninapo ona dhambi zangu, nisaidie niweze kuziungama niweze kuwa huru na sio aliye elemewa na mzigo wa dhambi. Bwana, ninaomba niyalinde maisha ya aina zote. Ninaomba nijitahidi kuwa mjumbe wa maisha. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni