Jumatatu. 25 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Februari 05, 2020

Februari 5,2020
JUMA LA 4 LA MWAKA

2Sam 24:2.9-17
Zab 32:1-2.5-7
Mk 6: 1-6.

MAMBO YA KAWAIDA YANATUFANYA TUWE TAYARI KUPOKEA YASIO YA KAWAIDA!

Watu waliokuwa wanamfahamu Yesu tangu akiwa kijana wanashangazwa na hekima na mambo makuu anayotenda. Walishangazwa na yote aliokuwa akisema na kutenda. Walikuwa wakimfahamu tangu alivyokuwa anakuwa, walifahamu wazazi wake na ndugu wengine, na kwa mshangao wanashangaa inawezekanaje huyu jirani yao wanaye mfahamu inawezekeanaje awavutie watu hivi na kuwa na hekima ya hali ya juu namna hii na matendo makuu. Ni wazi kwamba Yesu aliishi maisha ya kawaida kabla ya kuanza utume wake. Kiasi kwamba watu wake wa karibu hawakufahamu kwamba alikuwa mtu muhimu sana. Hili ni wazi kwasababu baada ya Yesu kuanza utume wake wa hadharani watu wake wanashangazwa na matendo yake makuu. Hawakutegemea kabisa mambo kama haya kutoka kwa Yesu wa “Nazarethi”.

Je, sisi tunaweza kupata nini kutokana na jambo hili? Kwanza kabisa tutambue , mara nyingi mapenzi ya Mungu kwetu yanatuita kuishi maisha ya “kawaida” kabisa. Ni rahisi kuwaza kwamba tunapaswa tutende mambo makuu kwa ajili ya Mungu. Lakini vitu vikubwa ambavyo Mungu anatuitia nikuishi maisha ya kila siku ya kawaida vizuri. Hakuna wasiwasi kwamba wakati Yesu alivyokuwa akiishi maisha ya kawaida alikuwa anaishi maisha ya fadhila. Haikuwa mpango wa Mungu kwanza fadhila zake zianze kujulikana kwanza kwa wote kipindi hicho. Pili, tunaona wazi kwamba kuna wakati utume wake ulibadilika. Mapenzi ya Baba, katika maisha yake, alianza utume wake hadharani na watu wakamuona. Na wakati hili lilivyo anza watu walitambua.

Ukweli huu pia ni dhahiri pia kwetu sisi. Watu wengine wameitwa maisha ya kawaida katika hali ya kawaida kabisa. Tambua kuwa muda huu ndio muda ulioitwa ili kukuza fadhila zako, fanya mambo ya kawaida kabisa vizuri, na furahia hali ya ukimya ya maisha ya kawaida. Pia tutambue kuwa kuna uwezekano Mungu akatuita katika maisha hayo ya kawaida na kuanza kumshuhudia mbele ya watu au umati. Ufunguo ni kwamba sisi tunapaswa kumsikiliza na kuitambua sauti yake katika hali ya utulivu. Kuwa tayari na penda yeye akutumie kwa jinsi alivyopenda kwa mapenzi yake ya Kimungu.

Leo tutafakari, juu ya mapenzi ya Mungu katika maisha yetu sasa. Anataka nini kutoka kwetu? Je, anatuita kutoka katika hali yetu ya kawaida ili tuweze kuishi maisha ya kumshudia yeye mbele za watu? Au anatuita sasa tuishi maisha ya kawaida katika hali ya ukimya ya kawaida na kupalilia fadhila kwanza? Furahia mapenzi yake kwa jinsi atakavyo penda uwe na kumbatia hilo kwa moyo wote.

Sala:
Bwana, nakushukuru kwa mpango wako kamili katika maisha yangu. Ninakushukuru kwa hali mbali mbali ulizoniita ili nikutumikie. Nisaidie daima niweze kuwa wazi katika mapenzi yako na daima niseme “Ndio” kwako, bila kujali unataka nifanye nini. Yesu nakuamini wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni