Jumapili, Januari 19, 2020
Jumapili, Januari 19, 2020.
Juma la 2 la Mwaka A wa Kanisa
Is 49: 3, 5-6;
Zab 40: 2-10;
1Kor 1: 1-3;
Yn 1: 29-34.
MUNGU ANAYEITA!
Karibia kila ukurasa katika Maandiko Matakatifu unaongelea kuhusu Mungu anayetuita sisi. “Hapo mwanzo Mungu aliviita viumbe vyote viwepo (Hek 11:25), alimwita mwanadamu kuja katika uzima na Adamu alivyo asi, alimuuliza uko wapi? (Mwa 3:9). Mungu aliwaita watu na akawapendelea kuliko watu wote wa ulimwengu (Kumb 10:14-15). Alimwita Abrahamu, Musa, na manabii na kuwapa utume waweze kuleta matunda, ili mpango wa ukombozi uweze kueleweka. Hakuna mtu wala kitu kisicho kuwa na umuhimu, kila mtu na kila kitu kina kazi yake ya kufanya. “Yesu anatuita kwa wito mtakatifu” (2 Tim 1:9). “Ametuita kwa njia ya Injili tunayo hubiri, kwani alitaka tushiriki utukufu wa Kristo Yesu Bwana wetu” (2 Thes 2:14).
Katika somo la kwanza, tunamsikia Bwana akimwambia Isaya. “wewe ni Mtumishi wangu, Israeli, kwa njia yake nitatukuzwa”. Katika hali ya kibinadamu ya kukata matumaini, Israeli aliye mdogo na mwaminifu anaitwa na Bwana. Anawakabidhi kazi mbili kubwa: kuwaunganisha watoto wa watu wake, waliotawanyika kati ya mataifa, na kuwarudisha katika ardhi ya Baba zao na kuwa mwanga na wokovu kwa miisho yote ya mataifa. Wakristo wazamani waliona kabisa sifa hizi za “mtumishi” zikijionyesha kwa Yesu. Kama “mtumishi” Yesu alifanya kazi yake akiwakusanya kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea (Mt 10:6). Alitamani mwanga wake uangaze zaidi ya wote katika Galilaya: “katika nchi ya Zabuloni na Naptali” watu wanaoishi katika giza wameona mwanga mkuu (Mt 4:15-16).
Katika somo la pili kutoka katika waraka kwa Wakorinto, Paulo anajionyesha mwenyewe kama Mtume kwa utume wake. Mtume ni yule anayetumwa ili aende kuhubiri Injili ambapo hakuna aliyeenda kutangaza, ni yeye aliye sia mbegu ambayo ilichipua na kumea, kukuwa na kuchanua na kuendelea katika jumuiya kubwa. Zaidi sana katika barua yake, Paulo anatumia picha hii “niliotesha, Apollo akamwagilia, Mungu ndiye aliyesababisha kukuwa na kuchipua. (1 Kor 3:6). Tofauti ya marabii na walimu wa kipindi hicho, Paulo hajisifii elimu yake, wala hekima yake, wala uzoefu alioupata kwa miaka mingi. Anongelea wito wake alioupokea kwa Mungu. Paulo alichaguliwa akapewa kazi, kuwa mtume. Anakumbuka wito huu ili Wakarintho waweze kukubali maneno yake, ujumbe wake na kuamua. Haelezei mambo yake binafsi, anaongea kwa neno la Mungu aliyemtuma.
Yohane katika Injili yake, anamuongelea Yohane Mbatizaji, kama “mtu aliyetumwa na Mungu kuwa shuhuda wa nuru” (Yn 1:6-8). Maisha yake na mahubiri yake yalisababisha maswali, matarajio na matumaini kwa watu. Kwa kumuona Yesu anakuja kwake, Yohane anasema “Tazama Mwana-kondoo wa Mungu, aondoae dhambi za ulimwengu (mstari. 29).
Hakukuwa na mtu yeyote katika Agano la Kale aliyeitwa “Mwana-Kondoo wa Mungu” Mwisraeli mwema, Yohane anatambua wasikilizaji wake, wakisikia juu ya msisito juu ya Mwana-Kondoo wa Mungu, wataelewa kwa haraka maana ya Mwana-kondoo wa Pasaka ambaye damu yake, iliwekwa katika kingo za milango katika nyumba huko Misri, iliowakomboa wazee kutoka katika upanga wa yule Malaika. Yohane Mbatizaji aliiona bahati ya kuwako Kristo. Kwamba siku moja atatolewa sadaka, kama Mwana-Kondoo, na damu yake itaondoa uovu wote na nguvu zote za uharibifu. Damu yake itamuokoa Mwanadamu kutoka katika dhambi na mauti.
Yohane Mbatizaji pia akilini mwake pia alikuwa na mwana-kondoo yule wa sadaka ya Abrahamu. Isaka akiwa anatembea pembeni njiani na Baba yake kwenda mlima Moria, aliuliza: “moto na kuni zipo, lakini yu wapi kondoo wa sadaka?” Abrahamu akajibu: “Mungu mwenyewe atatupatia Mwanangu”. Yohane mwenyewe anajibu sasa. Ni Yesu, tuliopewa sisi kutoka kwa Mungu kuja Ulimwenguni kuwa sadaka badala ya Mwanadamu mdhambi kupata adhabu.
Matazamo aliokuwa nao Yohane Mbatizaji kuhusu Yesu, unavutia sana na ni fumbo na linashangaza sana. Huenda Yohane alisoma Maandiko matakatifu ya kipindi chake, na huenda alijua vifungu vingi vinavyo husu ujio wa Masiha vilivyo ongelewa na manabii wa zamani. Huenda alijua Zaburi na Kitabu cha Hekima. Lakini, kwanza kabisa, Yohane huenda alijua aliokuwa anafahamu kwa zawadi ya Mungu ya Imani. Huenda alikuwa na mtazamo huo wa kiroho kama zawadi kutoka kwa Mungu. Ukweli huu haufumbui tu ukuu wa Yohane na undani wa Imani yake, bali anakuwa mfano ambao sisi tunapaswa kuufuata katika maisha. Tunapaswa kutembea katika mwanga wa kweli wa Mungu aliotupa katika maisha yetu kwa njia ya Kristo.
Yohane alijazwa kabisa na Hekima, akili, shauri, nguvu, na uchaji. Zawadi za Roho Mtakatifu zilimsaidia kuishi maisha ya neema za Mungu. Yohane alifahamu vitu na kuvielewa ambavyo ni Mungu pekee angeweza kuvifunua. Yohane alimpenda na kumheshimu Yesu kwa moyo wote na majitoleo ya nafsi yake ambayo yangeweza kufunuliwa na kupewa na Mungu. Ukweli wa hakika ni kwamba, utakatifu wa Yohane ulikuja kwasababu ya muunganiko wake na Mungu.
Leo tutafakari juu ya Mungu aliyewaita Paulo, Yohane Mbatizaji, na ambaye anaendelea kutuita kila mmoja wetu. Kama Yohane na Paulo, waliotambua kuwa Mungu anaishi na yupo katika maisha yao akiwaongoza na kuwafunulia ukweli wa Ufalme wake. Tujitoe leo, kuiga Imani ya ndani ya Yohane Mbatizaji na kuwa wazi kwa yale Yote ambayo Mungu anataka kuongea nasi.
Sala:
Yesu na Bwana wangu, naomba unipe utambuzi na hekima niweze kukutambua wewe na kukuamini wewe. Nisaidie mimi, kila muda na kila siku, niweze kutambua kwa undani kabisa fumbo la jinsi ulivyo. Ninakupenda, Bwana wangu, ninakuomba niweze kukupenda na kukufahamu wewe zaidi na zaidi. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni