Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Januari 13, 2020

Jumatatu, Januari 13, 2020
1Sam. 1:1-8
Zab. 116:12-14, 17-19 (K)
Mk 1: 14-20.

WITO WA MUNGU UNADAI UKARIMU.

Katika Injili tunamsikia huyu mpendwa wa Mungu (Yesu) akianza kazi yake, baada ya ubatizo wake. Yeye alikuja kwa lengo la kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu. Yeye aliona haja ya wafuasi wake kuendeleza dira hii na dhamira ya utume wake. Yesu aliwaita watu wa kawaida ambao katika viwango vya binadamu walionekana hawafai kama vile Simoni na Andrea, Yakobo na Yohane lakini walijitoa wenyewe kwa ukarimu katika maisha mapya kwamba Yesu alikuwa wito wao wakufuata. Haikuwa rahisi lakini walijitoa. Ilikuwa ni maisha ya Injili. Walipata uzoefu wa maisha kwamba Yesu aliishi ndani yao na alikuwa wito wao wa kwenda na kuwa wavuvi wa watu.

Ukarimu na kujitoa wenyewe kwa wafuasi wa kwanza ni mwaliko kwa ajili yetu pia. Hata kwa udhaifu wetu wa kibinadamu Mungu anatupenda na anatutaka tuwe wanafunzi wake. Muda umefika sasa tuyaache maisha yetu ya zamani na tuamue kuishi maisha mapya ya Injili bila kujibakiza nakurudia ya zamani.

Sala:
Bwana, naomba nihisi upendo wako. Unifanye Niishi vyema wito wangu ulionipa. Yesu nakuamini wewe
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni