Jumamosi, Januari 11, 2020
Jumamosi, Januari 11, 2020,
Juma baada ya Epifania
1 Yoh 5:14-21;
Zab 149: 1-6,9;
Yn 3:22-30.
KUBAKI DAIMA KWAKULITAZAMA FUMBO LA NOELI
Kesho, kip indi cha Noeli kinaisha kwa sherehe ya ubatizo wa Bwana. Kuna hatari yakupoteza muelekeo wetu kwa Yesu kama ilivyokuwa kipindi cha noeli kwasababu kipindi hiki kinaisha. Kama ilivyo pengine wengi wetu tumesha haribu mipango yetu ambayo tulikuwa tumejiwekea mwaka huu mpya, mara nyingi tuna tabia yakusema “najiwekea” malengo badala ya “tunajiwekea” malengo.
Yohane Mbatizaji katika Injili anatambua nafasi ya Yesu. Yohane anatupa sisi msemo wa “Yeye aongezeke mimi nipungue”. Alijua kwamba yeye sio Masiha. Alitambua kuwa chochote kile alichofanya na kufanikiwa kilitakiwa kitoe sifa na njia kwa Masiha. Yohane alijutambua vizuri.
Changamoto kwetu pia ni sisi pia kujitambua. Tunapaswa kuacha kuyapa kipao mbele mambo yetu kwa nguvu zetu wenyewe na badala yake tujikabidhi mikononi mwa Mungu. Tunapaswa tutambue sisi ni wadogo na Mungu ni mkubwa wa yote. Tunapaswa tutambue kadiri tunavyo jinyenyekeza kwa kujishusha mbele ya Mungu, mapendo yetu kwake yanaongezeka.
Nyakati zetu ni rahisi kuwa wabinafsi sana kuliko hata kipindi chochote kile katika historia ya mwanadamu. Kwa upande mwingine tukiwa tumejikita na kujikabidhi kwa Yesu tusijisahau. Kama Yohane Mbatizaji, tunapaswa kuwa na utambuzi sahihi wa maisha yetu. Tunapaswa kutambua vipaji vyetu, zawadi alizotupa Mungu, na wito wetu katika kutimiza mpango wa Mungu katika Maisha yetu.
SALA:
Bwana Yesu, nivute karibu nawe zaidi, ili niweze kukuona wewe tuu. Ninaomba niishi maisha yangu, uhusiano mzuri na wengine, katika kazi zangu bila kupoteza muelekeo wangu kwako daima.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni