Ijumaa, Januari 10, 2020
January 10, 2020.
------------------------------------------------
IJUMAA, Baada ya Epifania
1 Yn 5:5-13;
Zab 147: 12-15, 19-20;
Lk 5:12-16.
HAKUNA ASIYE NA THAMANI MBELE YA YESU!
Mara nyingi tukisoma Biblia tunasikia kwamba Yesu aligusa watu. Yesu aliwagusa kwa mikono. Aliwagusa na kuwabeba watoto walioenda kwake. Aliushika mkono wa aliyekufa na kumuamuru aamke. Alifanyiza tope na kumpaka kipofu machoni na kumponyesha. Wenye ukoma walikuja kwake Yesu akanyoosha mkono wake na kuponya. Kwa kumgusa mtu mwenye ukoma Yesu aliivunja sheria ya Kiyahudi kuhusu kutokumgusa mtu mwenye ukoma. Wakati Yesu anaponya alikuwa anafanya kwa uwezo kama Mungu tofauti na manabii ambao hutumiwa na Mungu.
Wakoma walitengwa na jamii na walikuwa lazima watoe ishara kwa wengine ili wasije kuwasogelea. Hawakuruhusiwa kushika sahani au vyombo vinavyotumiwa na wengine. Hawakuweza hata kuchota maji kutoka katika chanzo kimoja na wengine. Kwasababu hawakuweza kufanya kazi na wengine walitegemea sana sadaka za watu. Hivyo Yesu baada ya kufika nje na kumgusa mkoma alihatarisha kuambukizwa. Igeweza kuelezwa na viongozi wa dini kwamba hata Yesu yeyote asimsogelee kwani amemgusa mkoma na kadiri ya sheria za Kiyahudi angepaswa kujitakasa kabla hajaingia hekaluni.
Mkoma katika Injili ya leo anafanya kitu ambacho hakitasahaulika. Ingawaje hakutegmewa kumsogelea Myahudi na zaidi saana Mwalimu, aliamini kwamba Yesu anauwezo wakuponya ukoma wake. Yesu alikuwa na huruma kwa wakoma. Alimpa kadiri ya jinsi alivyo oomba. Na kama somo la kwanza linavyosema kila anayemwamini Mwana anaukamilifu wa uzima. Huyu mkoma alimwamini Yesu na kupokea utimilifu wa uzima. Hivyo hakuna hata mmoja wetu ambaye hana thamani machoni pa Mungu.
Sala:
Ee Bwana kama wataka waweza kunitakasa. Kama wependa unaweza kunisamehe mimi dhambi zangu, kunitia nguvu na kunipenda mimi. Ninakuomba unisaidie niweze kuwa na huruma na mkarimu kwa wale ambao kwenye jamiii wanao onekana hawafai katika jamii. Yesu nakuamini wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni