Jumatano, Januari 08, 2020
Januari 8 2020
------------------------------------------------
JUMATANO, BAADA YA EPIFANIA
1 Yn 4:11-18;
Zab 72: 1-2, 10, 12-13;
Mk 6: 45-52.
KUTULIZA DHORUBA KATIKA MAISHA YETU!
Katika Epifania Yesu alijidhihirisha kwa mamajusi. Lakini tukio la mamajusi linapatika katika injili ya Mathayo pekee. Injili ya Marko inaongea namna nyingine ambayo Yesu amejidhihirisha kwa mitume wake. Mwanzo kabisa mitume walimfahamu Yesu kama Mwana wa Maria, mama wa kijijini ambaye mume wake ni Yosefu ambaye ni mseremala. Ni Yohane mbatizaji aliyemtambulisha Yesu kwa hawa mitume kama mtu ambaye ni wa pekee kabisa.: Mwana Kondoo wa Mungu. Wakati huu walishangaa na kujiuliza. Andrea na Simon, Yakobo na Yohane walimfuata Yesu, ambapo aliwachukua katika miji na vijiji alivyotembelea, akitangaza ufalme wa Mungu.
Marko anaoneshwa kuwa wa kwanza kuweka Injili katika maandishi. Na ananaandika Injili yake kadiri ya maelezo ya Simon Petro, ambaye anatambua maajabu aliotenda Yesu katika mashua yake. Nyota ilimtambulisha Yesu kwa mamajusi katika Injili ya Mathayo, ujio wa mkombozi. Katika Injili ya Marko, nguvu ya Yesu ya kutuliza maji na mawimbi, kuongeza mikate na samaki na miujiza mbali mbali alioifanya Yesu, inamtambulisha Yesu kama Mwokozi aliyekuja kuwatembelea watu wake katika sayari hii. Mwisho kabisa, kwa Mathayo na Marko, utambulisho mkubwa wa Yesu kama Mwana wa Mungu ni ufufuko.
Katika somo la kwanza leo, anaonesha jinsi Yesu alivyojidhihirisha kwake; ‘”wapenzi, ikiwa Mungu alitupenda sisi kwanza, sisi pia tunapaswa kupendana. Hakuna aliyemuona Mungu wakati wote, kama tukipendana Mungu anaishi ndani yetu na Upendo wake unakamilishwa ndani yetu.”
Hofu na wasiwasi ni kitu ambacho kinamkumba mnyama yeyote na hata mwanadamu. Leo wafuasi wanakutana na jambo lakutisha na wanajazwa na hofu kuu. Ingawaje wao walikuwa ni wavuvi, lakini walijazwa na hofu. Jambo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wao. Yesu anaifanya hofu yao ipotee na kutulia kama alivyofanya kwa bahari.
Kila mmoja wetu katika maisha yetu tunakutana na dhoruba katika maisha yetu. Ni nini siri ya wale wote ambao wanaweza kusimama nakuendelea mbele pale wanapokumbana na dhoruba? Sio pesa zao, wala sio marafiki zao, wala sio msaada wao wa familia. Ni kwasababu ya Imani yao kwa Yesu.
Sala:
Bwana, ninatambua kwamba umekuwa hai ndani ya maisha yangu mara nyingi. Nisaidie mimi niweze kusimama katika zawadi hiyo ya neema. Nisaidie mimi niweze kutambua uwepo wako wa daima katika maisha yangu, ukiwa kama wewe ni chemichemi ya neema zote. Wakati ninapojisikia kana kwamba umeniacha ninakuomba unipe akili ya kutambua kwamba wewe daima upo pamoja nami na unatembea nami daima. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
Maoni
Ingia utoe maoni