Jumapili. 24 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatatu, Novemba 07, 2016

Jumatatu, Novemba 7, 2016,
Juma la 32 la Mwaka wa Kanisa

Tit 1:1-9
Zab 23:1-6
Lk 17:1-6


SOMO LA MAISHA YA UFUASI

Kuna sheria tatu katika sehemu ya Injili leo. Zinaweza kuleta mabadiliko katika maisha ya muumini. Atakayefuata sheria hizi kikamilifu atafanya mabadiliko katika maisha yake.

Sheria hizi ni:

1.Dhambi haitabiriki kama Yesu alivyosema ‘makwazo hayana budi kuja’ kwa namna nyingine nisawa nakusema, vitu vinavyosababisha dhambi havina budi kuja. Lakini kuwaongoza wengine kwenye dhambi ni kitu kibaya kabisa.

2. Yesu alisema kwamba, kama mtu akikukosea umuonye, lakini akiomba msamaha, umsamehe, haijalishi ni dhambi kubwa kiasi gani, haijalishi ni jiwe kubwa kiasi gani aliloweka katika njia zetu
.
3. Imani ni ufunguo wa nguvu zote ulimwenguni. Mfuasi anapaswa kuwa na Imani sahihi. Msisitizo si juu ya Imani kiasi gani alionayo mtu, ni kitendo tu cha kuwa na Imani na kuishi nayo.

Yesu katika hali ya mfano anaongelea kuhusu kung'oa mti nakuutupa baharini. Wakati tunapopatwa na mambo ambayo hayawezekani katika maisha yetu, tunapaswa kutumaini nguvu ya Mungu ili tuweze kufanya yasiyowezekana.

Sala: Bwana, ongeza Imani yetu ili tuweze kujenga ufalme wako. Amina

Maoni


Ingia utoe maoni