Jumamosi, Januari 04, 2020
Januari 4, 2020.
------------------------------------------------
KIPINDI CHA NOELI
Somo la 1: 1 Yn 3:7-10 Yohane anatuambia kwamba tusimruhusu mtu yeyote atuangushe kwenye dhambi. Wito wetu ni kuishi maisha ya Kitakatifu, ni kuwa watakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu, mtu yeyote ambaye haishi kitakatifu wala ambaye hampendi ndugu yake sio mtoto wa Mungu.
Wimbo wa Katikati:. Zab: 98:1, 7-9 Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
injili: Yn 1:35-42 tunaona furaha ya Andrea baada ya kukutana na Yesu, inayomfanya kwenda kumwambia Simon, tumemuona Bwana, akampleka Simoni kwa Yesu.
------------------------------------------------
JE, YESU NI LENGO LA MAISHA YAKO?
Yohane Mbatizaji Mwanadamu kama sisi, angeweza kufurahi na kuona watu wote wanamkimbilia yeye na kumsifu yeye tu. Angeweza kufurahia kuchukua sifa zote nakuacha kuwaonesha watu kwa Yesu. Lakini hakufanya hivyo. Kilicho tokea ni kwamba Yohane alitimiza kazi yake vizuri sana. Kuandaa njia na kuwaongoza watu kwa Yesu wakati ulipotimia. Wakati Yohane alivyo waambia wafuasi wake wawili " Mtazameni Mwanakondoo wa Mungu" walianza kumfuata Yesu na kumuacha Yohane. Pengine angeweza kujisikia kupoteza mfuasi katika hali moja. Lakini hali hiyo ilikuwa ni furaha kwani alikuwa akitimiza kazi Yake ya kuwachukuwa wengine kwa Yesu.
Hivyo tunapaswa kuwa hivyo. Ni rahisi kuzama katika maisha katika hali moja. Ni rahisi kutaka watu wote wakusikilize sisi na tunapokuwa maarufu hatutaki kuachia. Lakini maisha ya ukristo hayana ubinafsi. Lazima kupenda na kuwaongoza kwa Yesu. Yohane alitengeneza mfano mzuri sana wa fadhila, tunaitwa tufanye hivyo. Kwa kuwaongoza wengine kwa Yesu tunakuwa na furaha ya ajabu na kuondoa ubinafsi wote.
Wakati wale wanafunzi wawili wa Yohane walivyo anza kumtafuta Yesu, Yesu alichukuwa jukumu la kuwakaribisha pia. Alikutana nao. Aliwauliza kati ya swali kubwa sana katika maisha. “mnamtafuta nani?” walikuwa wanatafuta nini kwa Yesu na walikuwa wana lengo ghani katika maisha? Yeu anatuita sisi "njooni nanyi mtaona" kwamba maneno yake ni ya milele.
Sala:
Bwana nisaidie nitafute njia ya kuwaongoza watu kwako. Nisaidie mimi niweze kujitoa sadaka kila wakati. Nisaidie niweze kutambua kikubwa ni kuhusu upendo na kuutumia upendo huu kuwaleta watu kwako kwa furaha na kujitoa. Yesu nakuamimi wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni