Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumamosi, Disemba 07, 2019

Jumamosi, Desemba 7, 2019,
Juma la 1 la Majilio

Isa 30: 19-21, 23-26;
Zab 147: 1-6;
Mt 9:35 - 10: 1, 6-8

KUISIKILIZA SAUTI YA MUNGU!
Katika somo la kwanza tunasikia: hata kama tukigeuka kulia, au kushoto, tutaisikia sauti nyuma yetu ikisema “Njia ni hii, ifuateni”, Nabii Isaya anawahakikishia watu kuwa kama watatafuta muongozo wa Mungu, watalipata jambo hili – “Njia ni hii, ifuate!”

Leo tuna adhimisha kumbukumbu ya Mt. Fransisko Ksaveri, msimamizi wa Misioni (utume). Hari yake ya kimisionari ya kuhubiri Injili ilimpeleka India, Japan na China. Mt. huyu alisikia sauti ya Mungu kupitia Mt. Inyasi ‘yamfaa mtu nini kuupata ulimwengu mzima lakini akapoteza roho yake?’ hapa Fransisko alijisikia kulazimika kusikiliza. Na hili lilimfanya “ahubiri Injili kama kazi yake na kujitoa” Fransisko alijisikia mwenye nguvu kwasababu alijiaminisha kwa Mungu na ndani ya Kristo.

Hatutakuwa huru kamwe mpaka pale tutakaposikia na kuitii sauti ya Mungu. Ni juu yetu kuweka vema akili zetu kuyakubali mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yetu, bila kujali ni kitu gani! Sisi sote tunakosea hapa na pale katika maisha. Baadhi yetu tunakosa muelekeo njiani na kukata tamaa. Sisi hatupaswi kukata tamaa tunapaswa kujipanga tena vizuri na kutilia maanani sauti ya Mungu ndani yetu na kuifuata.

Sala:
Bwana, ninakushukuru kwa zawadi ya maisha. Asante kwa kuja duniani na kuingia katika maisha yangu. Asante kwa furaha ya kukufahamu wewe na kukupenda wewe. Ninaomba nikuruhusu ubadili maisha yangu niendelee kukutafuta wewe na kukuonesha kwa wengine. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni