Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Disemba 06, 2019

Ijumaa, Desemba 6, 2019
Juma la 1 la majilio.

Isa. 29:17-24;
Zab 27:1,4,13-14;
Mt 9:27-31


KUTAMBUA UPOFU WETU!

Leo watu wawili vipofu wanaponywa katika Injili ya leo, si kwasababu waliomba, ni kwasababu Imani yao imefanya yawezekane. “je, una amini naweza kufanya haya?”Yesu aliuliza, ‘ndio Bwana” walijibu. “Na iwe hivyo kadiri ya Imani yenu” . Kama swali kama hilo “je, una niamini mimi?” tungeulizwa sisi leo, jibu letu lingekuwa nini? Sio swala la kujibu tu kwa maneno, bali kwa jinsi tunavyo enenda katika maisha yetu ya kila siku. Umuhimu wa kushuhudia Imani yao baada ya kufunguliwa macho ni hakika. Ingawaje Yesu aliwakataza vikali, hawa watu walitangaza maneno yake katika nchi nzima. Kuponya huku kama ilivyo miujiza mingine sio tu tendo la kuponya bali pia tendo la wokovu. Tukio hili halijafungwa kwa hawa watu wawili wa kipindi hicho na sehemu hiyo katika Israeli. Kwa maneno mengine, tukio hili lina nifundisha kitu kila wakati na lina ujumbe juu yangu nyakati zote.

Je, ninatambua upofu ndani mwangu? Je, ninamtambua Yesu kuwa anaweza kuniponya na nahitaji kumtafuta kila wakati aniponye? Kama inavyo inyo onekana katika wimbo wa katikati leo “mwanga na wokovu wetu” upo tu kwa Bwana ambaye anaweza kutupatia mwanga huo wa ndani. Tunapaswa kutambua na kuona ukweli kuhusu sisi wenyewe, ili kwa Imani na unyenyekevu, tuweze kumuomba atuponye upofu wetu wa ndani.

Sala.
Bwana, nisaidie mimi niweze kushirikisha furaha ya kukuona wewe kwa wengine. Ninaomba furaha hiyo itiririke katika maisha yangu ili wote waweze kukushuhudia. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni