Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Novemba 29, 2019

Ijumaa, Novemba 29, 2019,
Juma la 34 la Mwaka

Dan 7: 2-14;
Dan 3: 75-81 (K) 59;
Lk 21: 34-36.


UPENDO WA KWELI UNASHINDA HOFU!

Katika Injili ya Leo Yesu anasema moja kwa moja kwamba Ufalme wa Mungu upo karibu. Ni karibu sana na pia upo mbali sana. Upo karibu katika hali mbili. Kwanza, kwamba Yesu atarudi katika utukufu na kufanya vitu vyote upya. Na kwamba ufalme wake wa milele utaanzishwa. Pili, ufalme wake upo karibu katika hali ya sala. Yesu anataka kukaa ndani mwetu na kuanzisha ufalme wake ndani mwetu, kama tutamkaribisha. Lakini mara nyingi hatupendi kumkaribisha katika akili zetu na mioyo yetu na wala hatutaki kuingia katika mapenzi yake matakatifu na makamilifu. Tunakuwa na wasi wasi sana kumkaribisha yeye aje akae ndani ya mioyo yetu na kumruhusu aanzishe ufalme wake ndani yetu.

Je, unatambua ni kwa jinsi ghani Ufalme wake ulivyo karibu yetu? Je unatambua ni kwa njia ya sala na mapenzi mema? Yesu yupo tayari kuja kwetu na kumruhusu yeye aongoze maisha yetu kama tutamruhusu. Yeye ni Mfalme mwenye nguvu kama tutamruhusu yeye atubadilishe kuwa viumbe vipya. Yeye anaweza kuleta Amani kamili na umoja katika roho zetu. Yeye anaweza kufanya makubwa na mazuri ndani ya mioyo yetu. Tunapaswa tu kusema neno na yeye atakuja ndani mwetu.

Kama tunavyofahamu kupuputisha kwa mtini ni alama ya kuja kwa kpindi cha ukame, tunaweza kusoma alama za nyakati, na wakati wa mwisho utakavyo kuja, tutakuwa tayari, kwani sisi tunalindwa na Kristo, kwani hakuna kitakacho tutenga na Upendo wa Kristo, sio hata mwisho wa dunia au nyakati. Yesu alisema kwamba “mbingu zitapita na dunia itapita lakini neno langu halitapita kamwe.”

Tafakari leo juu ya tamaa ya moyo wa Yesu wakutaka kuja nakuanzisha ufalme wake katika maisha yako. Anatamani kuwa kiongozi wako na kukuongoza moyo wako katika umoja na upendo. Mwache yeye aje na aanzishe ufalme wake ndani mwako.

Sala:
Bwana, ninakualika wewe na kukuita uchukue nafasi katika moyo wangu. Ninakuchangua wewe kama Bwana wangu na Mungu wangu. Ninakupa maisha yangu uniongoze kama unavyo penda Mungu na Mfalme wangu. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni