Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumapili, Novemba 24, 2019

Jumapili, Novemba 24, 2019.
Juma la 34 la mwaka c wa Kanisa

Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristo Mfalme

2Sam 5:1-3;
Zab 122:1-5;
Kol 1:11-20;
LK 23:35-43.

MFALME KATIKA UTAWALA WAKE.

Hadithi moja ya Ireland, inaeleza wakati ambapo nchi ya Ireland ilitawaliwa na wafalme. Mflame aliyekuwa anatawala hakuwa na mtoto wa kuirithi enzi yake. Hivyo, aliwatuma wajumbe wake kutangaza ujumbe wake katika kila mji na kijiji cha utawala wake. Aliwaalika vijana waliohitimu kwa mkutano na Mfalme. Mfalme alihitaji sifa mbili: mtu lazima awe na upendo wa kina kwa Mungu na kwa jirani yake.

Kijana mmoja alisikia tangazo hilo. Kwa hakika alikuwa na upendo wa dhati wa Mungu na kwa jirani. Lakini, alikuwa ni maskini sana, na hakuwa na mavazi ya adabu ya kuvaa katika mkutano na hakuwa na fedha za kununulia mahitaji muhimu kwa ajili ya safari ndefu kwenda kwenye ngome ya Mfalme. Aliamua kwenda kuomba nguo na mahitaji aliyotaka. Kila kitu kilipokuwa tayari, alianza safari yake. Baada ya mwezi mmoja wa safari, alifika karibu na ngome ya Mfalme, alimwona maskini mwombaji akikaa kando ya barabara. Mwombaji alinyanyua mikono yake juu akiomba msaada. “nina njaa na kujisikia baridi?” alisema kwa sauti ya kutetema, Je! unaweza kunipa kitu chochote nipate kula na nguo kuvaa? Kijana yule alivutwa sana na mwombaji. Alizitoa nguo zake za nje na kubadilishana na nguo za mwombaji zilizochakaa na kuchanika. Pia alimpatia mwombaji yule mahitaji aliyokuwa amebeba kwa ajili ya safari. Hii hairidhishi sana alitembea na nguo zilizochakaa kwenda kwenye ngome ya Mfalme. Alipofika kwenye ngome ya Mfalme, askari alimchukua kumpeleka eneo la wageni. Baada ya muda mrefu aliongozwa kwenda kumwona Mfalme. Aliinama kifudifudi mbele ya enzi ya Mfalme na aliponyanyua kichwa juu hakuweza kuamini macho yake. Alipomuona mfalme alimwambia: “Wewe ulikuwa ni mwombaji kando ya barabara!” Hakika ni kweli” alisema mfalme, “Nimetaka kujua zaidi kama hakika wampenda Mungu na jirani.”

Hadithi hii hakika inalingana na liturujia ya leo. Mfalme wetu ni Mfalme mwenye Upendo. Anatupenda sisi bila kikomo kwamba yeye alikuwa tayari kutoa utukufu wake kutuokoa kutoka katika utumwa wetu wa dhambi. Ukweli alishuhudia Upendo. Je, sisi tunaweza kusikiliza sauti ya upendo wake. Je mambo yetu si juu juu kwake. Yeye ni Alfa na Omega wa Upendo. Toka kwake huanza upendo na pia kwake yeye upendo huishia kwa ukamilifu. Tukiwa wafuasi wa Kristo Mfalme tukumbuke kwamba mwishoni mwa maisha yetu, tutahukumiwa juu ya upendo pekee. Kwa hiyo, tunajaribu kuwa waaminifu kwa Ufalme wake wa Upendo. Lirtujia. Bwana wetu Yesu Kristo katika maisha yake hapa duaniani alikuwa kweli Mfalme, mwenye huruma kweli. Maisha ya Yesu yenyewe yalikuwa ni alama ya huruma, ambaye aliweza hata kusema akiwa juu ya msalaba “Baba uwasamehe kwani hawajui watendalo”.

Kila tunapofikiria picha ya Mfalme, tunakumbushwa kuhusu kuvalishwa taji, au kuwa na utawala. Picha hizi zinaleta katika akili yetu alama ya fahari na utukufu wa Kifalme. Lakini tunavyo ona katika Injili ya leo Yesu anatangazwa kuwa Mfalme, akiwa na taji la miiba, taji la mti (msalaba) na ufalme wa wale waliomkataa na kumsulubisha. Je, ufalme na utukufu upo wapi? Kujibu hili, lazima tuwe na mawazo tofauti na ufalme tunao waza na Ufalme wa Yesu Kristo.

Tunapotafakari kuhusu Mfalme katika Agano la Kale, taswira na picha inayokuja kichwani ni kuhusu Mfalme Daudi. Tunaona kwamba Daudi alipata heshima na msaada kutoka katika makabila yote yaliokuwa chini yake. Tunaona katika utawala wake, taifa la Israeli likiingia katika kipindi cha neema, baada ya kuwashinda mataifa ya jirani waliokuwa wapinzani wao, na kuweza kuongeza utawala wao. Daudi aliwashinda Wafilisti maadui maarufu wa Waisraeli na hapo akajipatia umaarufu mkubwa kutoka kwa watu wake.

Maoni


Ingia utoe maoni