Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumanne, Novemba 26, 2019

Jumanne, Novemba 26, 2019,
Juma la 34 la Mwaka wa Kanisa

Dan 2: 31-45;
Dan 3: 57-61 (K) 59;
Lk 21: 5-11.


KUJIANDAA KWA MWISHO WA ULIMWENGU

Vitu vyote vizuri vinafikia mwisho. Vyote vilivyo na mwanzo vina mwisho. Mungu aliweka mwanzo wa Ulimwengu huu, atasababsha pia mwisho wake. Masomo yetu yanatilia mkazo hili. Injili ina ujumbe unao fanana, inaelezea jinsi ya muda wa kutisha ulivyo karibu. Lakini Yesu anamalizia kwa namna tofauti akielekeza kwamba tusimame imara, tusitishwe na wala tusidanganywe na mafundisho tofauti. Kitu cha muhimu sio kitatokea nini bali ni jinsi ghani tunapokea kwa Imani na kuenenda kwa Imani kwa yanayo tokea? Haijalishi ni lini au ni namna ghani ulimwengu utakavyo ishia, tunatambua sisi wote karibuni au baadae, kila mtu atakumbana na mwisho wake (kifo) ambapo kila mmoja anapaswa kutoa hesabu ya maisha yake. Je, tumeishi kwa Imani? Kama ndio, tutakuwa tayari kwa ujio wa Bwana wetu, vichwa vyetu vikiwa juu!

Kwa kila mmoja wetu, kunaweza kuwa na “matetemeko, njaa, au mapigo” ambayo tunakutana nayo katika maisha. Mara nyingi yanachukuwa picha mbali mbali na huwa yanasababisha tabuu katika maisha yetu mara nyingine. Lakini hayapaswi kuwako. Kama tunaelewa kwamba Yesu anaona matatizo yeyote yale ambayo tunaweza kukutana nayo na tukiamini kwamba yeye mwenywe atatuandaa kwa kukutana nayo, tutakuwa na amani zaidi matatizo yatakapo kuja. Tutakuwa na nguvu ya kusema kwamba “kipindi hiki ni kipindi ambacho Yesu alisema tutakutana nacho”. Hali hii ya uelewa wa kwamba matatizo yatakuja yatatuandaa na kuwa na matumaini na imani.

Tafakari leo, juu ya njia mbali mbali ambazo unabii wa maneno ya Yesu yametimizwa kwako, katika maisha yako. Tambua kwamba Yesu yupo katikati ya hayo matatizo yanayo tokea, akikuongoza katika kutimiza kile ambacho tayari unacho kichwani kwako.

Sala:
Bwana, wakati ulimwengu wangu unaonekana kunifunika na kunitenga mimi, nisaidie kufungua macho yangu na kukuelekea wewe na kuamini juu ya huruma na neema yako. Nisaidie mimi niweze kutambua kwamba hutaniacha mimi na kwamba una mpango kamili wa kila kitu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni