Ijumaa. 18 Oktoba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Novemba 03, 2016

Alhamisi, Novemba 3, 2016,
Juma la 31 la Mwaka wa Kanisa

Flp 3:3-8;
Zab 104:2-7;
Lk 15:1-10


KUPOTEA NA KUPATIKANA!

Je ni ujumbe ghani anaotaka kutuambia Yesu kuhusu Mungu na ufalme wake katika mfano wa kondoo aliyepotea na shilingi iliyopotea? Wote wawili, Mchungaji na Mama mwenye nyumba, “wanatafuta mpaka wapate kilicho potea”. Wanatafuta bila kukata tamaa. Jambo jipya analotaka kutufundisha Yesu ni kwamba wadhambi ni lazima watafutwe warudi sio kuwaombolezea. Mungu hafurahii kupotea kwa mtu yeyote, bali anatamani wote wakombolewa wawe na uhusiano naye tena. Ndio maana jumuiya yote ya Mbinguni hufurahi juu ya mwenye dhambi mmoja anapopatikana na kurudisha uhusiano wake na Mungu kwa kutubu. Watafuta roho za waliopotea leo hii wanahitajika sana. Je, tunasali bila kuchoka na kutafuta kuwarudisha waliopotea katika njia ya kumwelekea Mungu? Au tunafurahia kupotea kwa mwenzetu? Kushindwa kufurahia mafanikio ya wenzetu ni dhahiri kwamba tunafurahia upande mwingine wa kupotea kwake. Daima tujifunze kuwarudisha watu kwa Mungu, tuwaombee na kuwatia moyo ili sote tushikane mikono tuende kwa Mungu.

Sala: Bwana, naomba mwanga wako uondoe giza ili kile kilichopotea kipatikane. Nijaze kwa upendo wako wakubadilisha mioyo yetu ili niweze kuwa na huruma kama wewe ulivyo na huruma. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni