Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Oktoba 18, 2019

Ijumaa, Oktoba 18, 2019.
Juma la 28 la Mwaka

Sikukuu ya Mt. Luka Mwinjili

2 Tim 4:10-17;
Zab 144:10-13, 17-18;
Lk 10: 1-9


KUBEBA USHUHUDA WA YESU KRISTO

Leo tuna mheshimu Mt. Luka Mwinjili. Luka ameandika moja ya Injili, alikuwa ni rafiki na Mt. Paulo walisafiri mbali na karibu kwenda kuhubiri Injili, na hatimaye kutoa maisha yake kama shahidi. Alifungwa kwa miaka miwili na baada ya kuachiwa inasemekana alisulubishwa karibu na Achaia akiwa anaendelea na kazi yake ya kimisionari. Alikuwa ni daktari, mwenye elimu, na alikuwa ni kutoka katika familia yenye uwezo. Aina ya maisha ya ushahidi aliyokufa inaonesha uamuzi wake wa kumchagua Kristo, tofauti na maisha mazuri aliyokuwa nayo.

Katika Injili, Luka leo anatuonesha tena wengine sabini ambao Yesu anawatuma baada ya kupokea maelekezo. Luka lazima atakuwa pia ni mmoja wapo wa Wafuasi waliotumwa kwa utume. Ni vigumu kwa mtu ambaye hakuwa karibu na Yesu kufahamu namna hiyo na kuweka katika mpangilio katika kumwelezea kama mtu mkamilifu. Sisi pia maagizo haya yanatolewa kwetu. Tunapaswa kujitoa kwa ufahamu wetu wote kuhubiri Ufalme wa Mungu na sio kuyumbishwa na vitu vingine vidogo. Kufanya haya ni lazima kusafiri na mwanga-chukua tu, vile vya muhimu na tuache nyuma yote ambayo yanaweza kutuharibu. Tunakaribishwa kufanya kazi hii, si kwasababu ya chochote tutakachopata kutokana nayo, bali kwa yale tutakayo wapa wengine bila malipo, bila kutegemea heshima fulani au malipo flani. Bwana anataka wafuasi wake wamtegemee yeye na sio kujitegemea wenyewe.

Luka atakuwa alielewa kwamba kukubali wito wa kuhubiri Injili na kuacha yote unahitaji sadaka kubwa. Na hivyo akafanya uchaguzi wa kuacha yote na kumfanya Kristo awe kila kitu kwake. Mungu alimtumia Luka katika hali nyingi na hasa alitumia elimu yake kama chombo ambacho Roho Mtakatifu alimvuvia na kuandika Neno la Mungu.

Kama Luka, tunaitwa na Mungu kumfuata yeye bila kujibakiza na kutumwa katika utume pekee wa kutangaza Injili. Tunapaswa kutoa vipaji vyetu, muda wetu, na maisha yetu kwa ajili ya Kristo ili aweze kututumia kama anavyopenda.

Sala:
Bwana, tunavyo mkumbuka huyu Mtakatifu wako mkubwa, Mt. Luka ninakuomba niweze kuiga mfano wake wa kujitoa kwa ajili ya Injili yako. Nitumie mimi Bwana wangu kama chombo chako kitakatifu na ninakuomba unipe nguvu ya kuyatoa maisha yangu bila kujibakiza. Yesu nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni