Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Alhamisi, Oktoba 10, 2019

Alhamisi, Oktoba 10, 2019.
Juma la 27 la Mwaka

Mal 3: 13-20
Zab 1: 1-4, 6 (K) Zab 40: 4;
Lk 11: 5-13.


OMBA, TAFUTA, BISHA HODI!

“Amini nawaambia, ombeni nanyi mtapokea, tafuteni nanyi mtapata, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kila aombaye, atapewa na kila atafutaye atapata na abishaye atafunguliwa mlango” (Lk11:9-10)

Mara nyingi Injili ya leo yaweza kutokueleweka. Wengi hufikiri kwamba tunapaswa kusali sana tena mno ndipo Mungu atakapo jibu sala zetu. Wegine waweza kufikiri kwamba Mungu hajibu sala zetu kama hatuja sali ya kutosha. Na wengine waweza kufikiri kwamba chochote tuombacho tunapaswa kuendelea kuomba daima mpka pale ambapo tutapewa.

Ni kweli kwamba tupaswa kusali daima na kwa kujitoa. Lakini cha muhimu kabisa cha kuelewa ni hiki: ni napaswa ni Sali kwa ajili ya nini? Hili ni muhimu kwasababu Mungu hatatupa kile tunacho omba, haijalishi ni mara ngapi umesali na kwa nguvu kiasi gani, kama hakipo kwa ajili ya mapenzi yake na utukufu wake. Kwa mfano, kama mtu ni mgonjwa na anakaribia kufa na ni sehemu ya mpango wa Mungu, wa Mungu mwenyewe wa kuruhusu huyo mtu afe, sala zote za ulimwengu haziwezi kubadili hili. Badala yake, sala kwa namna hii humwalika Mungu katika hali hii ngumu na kumjalia kifo kitakatifu. Hivyo sala sio hali ya kumbembeleza Mungu mpaka atupatie kile ambacho sisi tunataka, kama vile mtoto anavyoweza kufanya kwa mzazi. Bali tunapaswa kusali kwa ajili ya kitu kimoja tu na ni kimoja tu….. “mapenzi ya Mungu yatimizwe”. Sala hazisaliwi ili kubadilisha akili ya Mungu, ni kwa ajili ya kutubadili sisi na kukumbatia yote ambayo Mungu ametuita tuyanfanye.

Wengine wanasema “nimeomba kwa muda mrefu sana, lakini hakuna hata kimoja nimepewa” lakini katika kweli huwa tunatafakari na kujiuliza kama nimeomba kitu sahihi? Je nina tambua thamani ya vitu ninavyo omba? Je, vitu nilivyo viomba ni vya muhimu? Kama nitapewa je, nitaweza kuvitumia vizuri?

Mtoto asiye na meno anaweza kumuomba Baba yake mua. Je, Baba yake atampa? Hapana. Baba atasubiri mpaka akue awe na meno ndio ampe. Nyani hafahamu thamani ya dhahabu ulioshika. Lakini aweza kunyosha mkono kuomba, je utampatia? Hapana, haumpi. Kwasababu unafahamu thamani yake! Ni katika hali hiyo tunaweza tusijue tunanyoosha mkono kuomba nini, lakini Mungu anajua. Hii haimaanishi tusiombe chochote tunacho penda. Tunaweza kuomba lakini kama hatuvipati tunavyo omba, tusikatishwe tamaa. Mungu anajibu katika hali ambayo itakunufaisha na njia ambayo itakufanya ulicho omba kisikutenge naye.

Sala:
Bwana nisadie mimi daima nikutafute wewe na niweze kuongeza maisha yangu ya imani kwa njia ya sala. Ninaomba sala zangu zinisaidie kupokea mapenzi yako matakatifu katika maisha yangu. Yesu nakutumainia wewe.
Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni