Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Septemba 06, 2019

Ijumaa, Septemba 6, 2019.
Juma la 22 la Mwaka wa Kanisa
Sala ya Kanisa (Zaburi)-Juma la 2


Kol 1:15-20;
Zab 100: 1-5;
Lk 5: 33-39

Neema inayoshangaza
Katikasomo la kwanza tunaona wimbo wa Mt. Paulo. Wimbo huu uikuwa miongoni mwa nyimbo maarufu kwa wakristo wa kwanza. Wimbo huu unaelezea nafasi maalumu ya Yesu Kristo katika uumbaji, kichwa cha mwili yaani kichwa cha kanisa. Ni bahati iliyoje kwetu sisi kuwa sehemu ya mwili wake, yeye ambaye anatuunganisha kwa Mungu asiyeonekana, Baba wa wote.
Katika hali ya maisha yetu mambo yanaweza akutuendea mrama. Baadhi yetu wanapofurahia neema inayotolewa bila malipo na Mungu, wengine wanalalamikia matatizo waliyo nayo wanafunga na kusali kwa nguvu zao zote.maisha ya Yesu yalionekana kikwazo kwa wapinzani wake. Hata leo Yesu bado anapingwa. Yesu anawashutumu watu hawa na kuwaonya kama mzazi amwuonyavyo mwanawe anaposema kuwa “tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza! Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!”. Baadhi ya watu hawawezi kutambua neema ya Mungu iliyowazunguka.
Watu walio na mioyo migumu hukataa mabadiliko na hudhani kuwa neema ya Mungu yaweza kuwekwa chini ya nguvu za mwanadamu, hii ni kwasababu ya ugumu wa mioyo yao. Watu wa namna hii wanataka kuweka kiraka cha vazi jipya katika vazi kuukuu na kutia divai mpya viriba vya zamani. Viriba vya zamani vitapasuliwa na kani au msukumo wa divai mpya na kiraka cha zamani hakiwezi kuendana na rangi au aina ya nguo mpya.
Kuruhusu mabadiliko
Watu wanapotuingilia katika shughuli zetu za kila siku tunaweza kuwakatalia na kuwataka watuache tuwe huru. Kitu cha namna hii kinaonekana katika injili ya leo. Mafarisayo wanamuuliza Yesu kwanini wanafunzi wake hawasali kama mafarisayo lakini Yesu anawajibu kwa kupitia mfano wa divai na viriba.
Wapendwa, tunatakiwa kufanya kazi katika uwepo wa Kristo ambaye ndiye divai mpya. Tunatakiwa kutenda Zaidi ya mazoea. Yesu atatuongezea nguvu yeye mwenyewe na atatufanya tuwe na uhusiano bora na Mungu. Hivyo tuombe kwa ajili yetu wenyewe kuwa tayari na kujiandaa kupokea divai hii mpya.

Maoni


Ingia utoe maoni