Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Ijumaa, Agosti 30, 2019

Ijumaa,Agosti 30, 2019
Juma la 21 la Mwaka

1 Thes 4: 1-8;
Zab 96: 1-2, 5-6, 10-12;
Mt 25: 1-13
___________________

TAA IKIWAKA KWA “MWANGA WA UKARIMU”

Leo katika Injili tunaona hofu ya wanawali watano katika mfano wa wanawali kumi. Watano kati yao walikuwa wamejiandaa kumpokea Bwana wetu lakini wengine watano walikuwa hawaja jiandaa. Wakati Bwana wetu alivyokuja wale watano walikuwa mbali wakitafuta mafuta, na walipo rudi, mlango wakuingia karamuni ulikuwa umesha fungwa.

Yesu anatoa mfano huu ili kutuamsha sisi. Tunapaswa kuwa tayari kwa ajili yake kila siku. Na tutajuaje kwamba tupo tayari? Tupo tayari wakati tukiwa na “mafuta” yakutosha ya ukarimu kwa ajili ya taa zetu. Kwa hiyo swali dogo la kujiuliza ni kwamba, je mimi ni mkarimu katika maisha yangu?

Ukarimu sio kitu tu cha upendo wa kibinadamu. Sio kitu kinacho tokana na mvuto wa mwili au hisia au vitu vya watu. Ni zaidi. Ukarimu maana yake kupenda kwa moyo wa Kristo. Ukarimu ni zawadi ya Mungu inayotusaidia tutoke nje ya nafsi zetu na kwenda kuwasaidia wengine katika hali ambayo inapita hata uwezo wetu. Ukarimu ni tendo la Kimungu na ni muhimu kama sisi tunataka kukaribishwa katika karamu ya mbinguni.

Tafakari leo kama unaweza kuona moyo wa Yesu ukiwa ndani ya moyo wako leo. Je, unamuona yeye akiwa ndani yako akikuambia uende kukutana na watu hata pale ambapo unaona ugumu? Je, unatenda na kufanya mambo ambayo yanawavuta watu kuishi maisha ya kitakatifu? Je, Mungu anafanya kazi ndani yako na kwa kupitia wewe kuleta mabadiliko ulimwenguni? Kama jibu ni ndio basi ukarimu ni njia ya maisha yako.

Sala:
Bwana fanya moyo wangu kuwa sehemu yako ya kuishi. Ninaomba moyo wangu udunde kwa mapendo yako na ninaomba maneno yangu na matendo yangu yashiriki katika ukamilifu wako wa kuwajali wengine. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni