Alhamisi, Agosti 29, 2019
Alhamisi, Agosti 29, 2019
Juma la 21 la Mwaka
Kumbukumbu ya Kukatwa kichwa kwa Yohane Mbatizaji
MASOMO YA MISA
1 Thes 2: 1-8;
Zab 138: 1-3, 4-6;
Mk 6:17-29
TUSIMAME KWA UKWELI!
Ushahidi wa Mt. Yohane Mbatizaji unatukumbusha kwamba wito wa muhimu katika Ukristo wetu kuliko yote ni kuishi Injili. Hatuna wasi wasi kwamba Yohane aliteseka gerezani na kifungo kama shahidi wa mkombozi, yeye alikuwa ndio mtangulizi. Mtesi wake, mfalme Herode na Herodia hawakumuhukumu ili amkane Kristo, bali walitaka akae kimya kuhusu ukweli, afiche ukweli. Lakini hakuweza kukaa kimya. Na matokeo yake ilimbidi kukatatwa kichwa chake na watesi wake. Alikufa kwasababu ya ukweli, alikufa kwa ajili ya Kristo. Je, Yesu hakusema “mimi ni ukweli!” kwahiyo kwasababu Yohane alimwaga damu yake kwasababu ya ukweli ni wazi na hakika kwamba alikufa kwa ajili ya Kristo.
Je, tumekuwa waoga kufanya jambo sahihi au kutoa ushuhuda wa Imani yetu au kusimama kwa ajili ya ukweli kwasababu tulikuwa tunaogopa wengine wanatufikiriaje au watatuambia nini? Nina Imani kwamba wengi wetu tulishakuwa hivyo, ni kitu ambacho tunapigana nacho kila wakati. Vijana wanateseka kupita katika makundi mbali mbali na hujikuta wakiingia katika tabia mbali mbali zisizo nzuri, wakati mwingine hujikuta wanahatarisha maisha yao, chanzo ikiwa nikuogopa kusimamia ukweli. Wafanyakazi wanagoma kwa kutoa sababu za kupinga rushwa au tamaduni mbali mbali zisizo jali utu wa watu. Sisi Wakristo tunakuwa Wakristo wa jina tu sio wa matendo yetu. Ni kitendo cha vita kati ya dhamiri zetu na vionjo vyetu. Tuna mfano wa mfalme Herode, aliyejua kwamba kitu cha kweli cha kufuata ni kumsikiliza Yohane Mbatizaji na kumwachia huru, lakini alikuwa anaogopa wageni wake watamfikiriaje. Kinyume na nia yake nzuri, anamtoa Yohane auwawe. Yohane alitoa thamani ngumu, kwasababu alifanya uchaguzi sahihi wa kuwa mwaminifu kwa Bwana na akasimama kadiri ya ukweli wa dhamiri yake. Ushuhuda wa Yohane ni mfano kwetu wakusimama imara kila mara kwa kuchagua lililo sahihi kila mara na kulifanya. Ni wazi mbele ya macho ya watu tunaweza kuonekana wajinga, lakini mbele ya Mungu tutaonekana kama watakatifu.
Sala:
Bwana, tufanye waenezaji wa ukweli kwa maneno na matendo yetu. Bwana ninakuomba niwe na ujasiri wa Mwana wako na nguvu kama ya Yohane Mbatizaji katika kubeba misalaba yangu katika maisha. Ninakuomba nibaki imara katika sala nikiwa nimejazwa matumaini ninapo kusikia wewe ukiniita mimi kubeba msalaba wangu. Yesu, nakutumainia wewe.
Amina
Maoni
Ingia utoe maoni