Alhamisi. 16 Mei. 2024

Tafakari

Alhamisi, Juni 30, 2016

Alhamisi, Juni,30,2016,
Juma la 13 la Mwaka wa Kanisa

Amo 7: 10-17;
Zab 18: 8-11;
Mt 9: 1-8

NINI MAANA YA UKWELI?

Ingawaje mwanadamu anatafuta ukweli daima, lakini yeye mwenyewe ni sababu yakuto kuutambua. ‘Ukweli ni kitu ghani?’ swali maarufu lililoulizwa na Pilato ambalo hadi leo husikika masikioni mwetu. Lakini pilato hakuwa na subira (Yn 18: 38) yakutosha kusubiri jibu kutoka kwa Bwana wetu Yesu ambaye ni njia, ukweli na uzima. Sisi tunapenda sana kujua ukweli kuhusu wengine, sio tu kupenda bali tunapoteza muda mwingi kujaribu kutaka kujua ukweli kuhusu wengine. Lakini pia tunajaribu kwa njia zote kukwepa ukweli kuhusu sisi wenyewe! Ukimya ! tunachukia ukimya-kwasababu ukimya nisilaha kubwa ya kugundua ukweli. Ukweli unaweza kukutana nao moja kwa moja-kwanjia ya ukimya na tafakari au pia unaweza kufunuliwa na Mungu mwenyewe-ambaye ni Ukweli wote-kwa njia ya manabii, maandiko matakatifu au watu wake aliowachagua.

Katika somo la kwanza, tunapata tukio kama hilo ambapo nabii Amosi anashuhudia ukweli-mchanganyo uliopo katika kuabudu, katika maisha ya pamoja na maisha binafsi. Lakini anakataliwa na Amasia kuhani wa Betheli. Katika injili tunaona mtu aliyepooza analetwa kwa Yesu. Tofauti na madakatari wa sasa, daktari mkuu anamponya kabla ya kuuliza sababu. Kristo kamwe hakumponya mtu kabla hajampa ukombozi kwanza na msamaha. Leo tunaalikwa tuingie ndani ya nafsi zetu wenyewe tugundue ukweli kuhusu sisi wenyewe. Tufungue moyo wetu tupokee ujume wa Yesu na mpango wake juu yetu.

Sala: Bwana, naomba unisaidie niweze kukuona wewe ndani yangu nami ndani yako. Amina.

Maoni


Ingia utoe maoni