Jumanne. 26 Novemba. 2024

Tafakari

Jumatano, Agosti 21, 2019

Jumatano, Agosti 21, 2019
Juma la 20 la Mwaka
_______

Amu 9: 6-15;
Zab 20: 2-7;
Mt 20:1-16
_______

JE, UNAKUWA NA WIVU MWENZAKO ANAPO FANIKIWA?

Somo la Injili ni maelezo ya mfano wa wakulima katika shamba la mizabibu. Mfano unaeleza ni kwa jinsi ghani mwenye shamba alivyoenda sokoni kwa muda tofauti tofauti na kutafuta wafanyakazi hata wakati wa saa kumi na moja jioni. Wakati wale wafanyakazi wa kwanza walikuwa wamekubaliana kabisa kwamba watapewa mshahara wa dinari moja, na wakati wengine wakiambiwa watapewa kilicho haki yao. Wakati wa malipo macho yalikuwa kwa wale ambao wameajiriwa wa mwisho, wakati wale wa kwanza wakilipwa mbele ya wengine wote. Wa mwisho wanalipwa sawa kama walivyokubaliana na mwenye shamba. Ingawaje mfano hausemi ni kiasi gfhani cha kazi kilicho fanyika au pengine wale wa mwisho walifanya kazi haraka haraka kiasi cha kuwafikia wale wa kwanza? Hausemi. Hali hii inaleta changamoto! Lakini Yesu alitaka kusema kwamba wadhambi na watoza ushuru walio tubu watakuwa pia katika hali moja na wale ambao wameshika sheria tangu mwanzoni. Mfano huu unataka kutufundisha kitu kwamba, Mungu haangalii ni kwa muda ghani uliofanya kazi, bali ni kwa jinsi ghani ulivyo mwaminifu katika kazi.

Kwanza kabisa, hali hii inashawishi kila mtu kuwa na wivu. Wivu ni aina ya kuwa na huzuni au kutokufurahi kwasababu ya mtu mwingine kufanikiwa. Pengine tunaweza kuelewa wivu waliokuwa nao wale waliofanya kazi siku nzima. Ukweli si kwamba ni kitu ghani walichopokea bali ni wale wengine wamepokea kiasi hicho hicho kama wao, hivyo inaonekana kuwa kama sio haki. Tofatuti ni kwamba wale wa kwanza wamepokea kile walicho kifanyia kazi siku nzima, na wengine wamepokea sawa na hao wengine kwasababu ya ukaribu wa Bwana shamba.

Kama sisi tutajiweka na lile kundi linalo lalamika, ni vizuri tuangalie misukumo yetu. Je, sisi tunaweza kujazwa furaha na Amani kwasababu ya ndugu zetu kufanikiwa? Je, waweza kumshukuru Mungu na kumwambia asante wakati ndugu au mwingine alivyo fanikiwa? Wivu mbaya ni dhambi, na ni dhambi ambayo inatuacha tukiwa hatuja ridhika na wenye huzuni. Njia pekee ambayo tunaweza kushinda ni kufurahia mafanikio ya ndugu zetu.

Sala:
Bwana, ninatenda dhambi na ninakubali kwamba nina wivu moyoni mwangu. Ninakushukuru wewe kwa kunisaidia kuliona hili ninakuomba unisaidie sasa nikabidhi kwako. Tafadhali nisaidie kuondoa kwa kuwa na shukrani kwa neema na huruma yako unawajalia wengine. Yesu, nakuamini wewe.
Amina

Maoni


Ingia utoe maoni